Watu 16 wa mataifa ya kigeni wakamatwa nchini Uturuki kwa tuhuma ya ugaidi

Watu 16 wa mataifa ya kigeni wakamatwa nchini Uturuki kwa tuhuma ya ugaidi

Watu 16 kutoka mataifa ya kigeni nchini Uturuki wamekamatwa kwa tuhuma ya kuwa na fungamano na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yametangazwa na vyombo vya habari vya Uturuki na kusisitiza kuwa watu 16 ambao ni raia wa mataifa ya kigeni nchini humo wamekamatwa na majeshi ya ulinzi na uslama katika mikoa mbalimbali ya nchi hiyo.
Viongozi wa idara maalumu ya kupambana na matukio ya meripuko nchini Uturuki, kufuatia mpango maalumu wa mashambulizi dhidi ya vikundi vya kigaidi, siku mbili ziliopita wamefanikiwa kuwakamata watu 16 kutoka mataifa mbalimbali kwa tuhuma ya kuwa na fungamano na kikundi cha kigaidi, imeelezwa kuwa watu 3 miongoni mwa waliokamatwa ni raia wa Iraq na wengine waliobaki ni raia wa Syria.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky