Watu 22 wauwawa na kujeruhiwa kufuatia mripuko wa kigaidi magharibi mwa Iraq

Watu 22 wauwawa na kujeruhiwa kufuatia mripuko wa kigaidi magharibi mwa Iraq

Kufuatia mripuko wa kigaidi uliotokea katika mji wa Hit katika mkoa wa Anbar umepelekea watu 22 kuuwawa na kujeruhiwa nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kutokea kwa mripuko wa kigaidi nchini Iraq zatangazwa, ambapo gaidi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh alijiripua jana jumatano katika mjumuiko wa watu ambao walikuwa wakinywa Kahawa katika sehemu ya Dawareh iliopo katika mji wa Hit katika mkoa wa Anbar nchini Iraq.
Katika shambulio hilo watu 7 waliwawa papohapo na wengine 15 kujeruhiwa na kukimbizwa Hospitali kwaajili ya matibabu.
Majeshi ya serikali ya Iraq hivi mwishoni yamefanikiwa kuukomboa mji wa Hawij uliopo katika mkoa wa Kirkuk kaskazini mwa Iraq ambapo magaidi wa Daesh wamesambaratishwa kikamilifu katika sehemu hiyo.
Majeshi ya Iraq hivi karibuni yamefanikiwa kuikomboa sehemu kubwa ya ardhi hiyo ambayo ilikuwa imetekwa na magaidi wa Daesh kiasi kwamba mpaka sasa kikundi cha kigaidi cha Daesh kinamiliki sehemu ndogo iliopo katika mkoa wa Anbar magaharibi mwa Iraq.
Mkoa wa Anbar nchini Iraq ndio mkoa mkubwa zaidi nchini humo, ambapo umepakana na nchini tatu Syria, Jordan na Saudi Arabia.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky