Waumini Izadi 36 wakombolewa kutoka mikononi mwa Daesh

Waumini Izadi 36 wakombolewa kutoka mikononi mwa Daesh

Idadi kadhaa ya wanawake na wanaume wakiwemo na watoto wa dini ya Izadi baada ya kukombolewa kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh wameamishiwa katika vituo vya jumuia ya Umoja wa mataifa katika sehemu ya Dahok iliopo katika sehemu wanayoishi Wakurdi nchini Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jumuia ya umoja wa Mataifa imetangaza kukombolewa kwa waizadi 36 ambao ni miaka mitatu sasa walikuwa wametekwa na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq.
Ofisi ya umoja wa mataifa inayosimamia masuala ya misaada ya kibinadamu imetangaza kuwa, miongoni mwa waliokombolewa ni wanawake, wanaume na watoto ambao mpaka sasa wamefikishwa katika vituo vya jumuia hiyo sehemu ya Dahok katika maeneo wanayoishi wakurdi nchini Iraq.
Kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa ni kwamba watu hao mpaka sasa wamepatiwa huduma za matibabu na masuala ya kiseikolojia na kupewa mssaada wa kuonana na familia zao.
Jumuia ya umoja wa Mataifa mpaka sasa haijafafanua kuwa watu hao wakombolewa kwa njia gani, hii ni kwa sababu ya hifo ya kuingia dosari kunako suala la juhudi za kuachiwa huru kwa waizadi waliopo mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh baada ya kuuteka mji wa Sinjar mwaka 2014 walifanya mauaji ya kinyama dhidi ya wafuasi wa dini ya Izadi na wengi kuwateka.
Majeshi ya wakurdi ya sehemu hiyo mnamo mwaka 2015 kwa mara nyingine walifanikiwa kuukomboa mji huo kutoka mikononi mwa kikundi hicho, ama baada ya kuikomboa sehemu hiyo walikuta idadi kubwa ya waumini wa dini ya Izadi walitekwa katika kipindi ambacho magaidi hao walikuwa wako katika sehemu hiyo.
mwesho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky