Waziri Malaysia akosoa marufuku ya Hijabu kwa wanawake wafanyao kazi hotelini

  • Habari NO : 867304
  • Rejea : IQNA
Brief

Waziri huyo ameshangaa ni kwa nini wanawake wanayimwa haki ya kuvaa Hijabu na kusema: "Ni jambo lisilokubalika. Hijabu ni haki ya wanawake. Nashangaa ni kwa nini wanawake walio katika receptionist za baadhi ya hoteli wanazuiwa kuvaa Hijabu."

Amesema Malaysia ni nchi ambayo wanawake wengi wanavaa Hijabu ni hivyo hilo halipaswi kuwa suala lenye mjadala.

Waziri huyo ametoa tamko hilo baada ya kubainika kuwa mahoteli maarufu Malaysia yanawazuia wanawake wenye kuvaa Hijabu kuwa katika maeneo ya kuwapokea wageni.

Jumuiya ya Wafanyakazi Malaysia hivi karibuni ilisema wafanyakazi wengi wanalalamika kuwa wanazuiwa kuvaa Hijabu wanapofanya kazi katika baadhi ya hoteli kubwa nchini humo.

Malaysia ni nchi ya Kiislamu ya Asia ya kusini-mashariki kando ya Bahari ya Kusini ya China na dini rasmi nchini humo ni Uislamu ambapo karibu asilimia 65 ya wakaazi wote milioni 32 nchini humo ni Waislamu.
............
300


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky