Waziri mkuu wa Iraq: kuangamiza ugaidi kutapatikana kwa kusambaratisha fikra zao

Waziri mkuu wa Iraq: kuangamiza ugaidi kutapatikana kwa kusambaratisha fikra zao

Adil Abdul-Mahdi waziri mkuu wa Iraq amesisitiza kuwa ili tuweze kuusambaratisha ugaidi awali tunapaswa kuisambaratisha itikadi na fikira za kigaidi

Shirika la habari AhlulByat (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na Adil Abdul-Mahdi, waziri mkuu wa Iraq katika kikao chake na makamanda wa ulinzi na usalama wa nchi hiyo na sisitiza kuwa vita dhidi ya ugaidi ni bado yenye kuendelea.
Aidha amesema: fikra ya kigaidi bado inaonekana bado ingalipo katika jamii yetu, ambapo inahitajia mpango kabambe wa kukabiliana na fikika hiyo hatimayae kuisambaratisha.
Wazi mkuu wa Iraq ameendelea kusema kuwa: majeshi ya ulinzi na usalama yanapaswa kuendelea kuwasaka magaidi waliobaki nchini Iraq kwa kufanya mashambulizi mbalimbali katika maficho yao.
Waziri huyo ameviita vikundi vya kigaidi vya Daesh na vyengine kuwa ni Saratani, na kusema kuwa ili kuusambaratisha ugonjwa huo tunalazimika kuisambaratisha fikira hiyo katika jamii ya kibinadamu.
Kamanda wa ulinzi na usalama wa majeshi ya Iraq naye alizungumza katika mkutano huo na kutoa ripoti ya hivi mwishoni ya masuala ya ulinzi na usalama ya nchi hiyo hasa kunako maeneo ya mipaka ya nchi hiyo na Syria.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky