Waziri wa mambo ya nje wa Iraq atarajia kwenda Syria

Waziri wa mambo ya nje wa Iraq atarajia kwenda Syria

Waziri wa mambo ya nje wa serikali ya Iraq kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu ametangaza safari ya siku mbili nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri wa mambo ya nje nchini Iraq ametangaza safari yake nchini Syria ikiwa ni kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka mitatu, ambapo atafanya ziara ya siku mbili nchini humo, naye ataonana na viongozi wa nchi hiyo na kufanya mazungumzo hususan kunako mabadiliko na matatizo ya ukanda wa mashariki ya kati na kukuza fungamano baina ya mataifa hayo.
Kwa upande mwingi wizara ya mambo ya nje ya Syria imetanga safari ya waziri huyo wa Iraq nchini humo ama haijatoa ufafanuzi kuwa safari hiyo itakuwa mnamo tarehe ngapi!.
Aidha Walid Al-mualim, waziri wa mambo ya nje wa Syria mwezi ulipita alimtaka waziri wa mambo ya nje wa Iraq kwenda nchini mwake na kufanya mazungumza katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Safari ya mwisho ya waziri wa mambo ya nje wa Iraq nchini Syria ilikuwa ni mwaka 2015 ambapo walikuwa wamezungumzia jinsi gani ya kupambana na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika nchi hizo.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky