Waziri wa mambo ya nje wa Saudia: Saad Hariri hajakamatwa

Waziri wa mambo ya nje wa Saudia: Saad Hariri hajakamatwa

Adel al-Jubeir waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia amesema: madai yakuwa Saudi Arabia amemlazimisha Saad Hariri (waziri mkuu wa Lebanon) kujiuzulu, ni madai yasiokuwa na msingi na hayaleti maana.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia “Adel al-Jubeir” amesema kuwa madai yakuwa serikali ya Saudi Arabia amemlazimisha waziri mkuu wa Lebanon (Saada Hariri) kujiuzulu ni madai yasiokuwa na msingi na hayana maana.
Aidha waziri huyo amedai kuwa kikundi cha Hizbullah nchini Lebanon ndio chanzo cha matatizo ya kisiasa nchini Lebanon,
Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia ameendelea kusema alipokuwa anahojiwa na Televishen ya CNN kuwa kikundi cha Hezbullah nchini Lebanon ndio iliosambaza suala hilo, kwani Hezbullah kinatishia viongozi wa serikali ya Lebano ndio ikatangaza kuwa Saudi Arabia ndio iliomlazi Saad Hariri kujiuzulu katika nafasi yake ya uwaziri mkuu wa Lebanon.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky