Wilaya ya Punjab nchini Pakistani yazuia kufanya maombolezo ya Bibi Fatimah Zahra (a.s)

Wilaya ya Punjab nchini Pakistani yazuia kufanya maombolezo ya Bibi Fatimah Zahra (a.s)

Viongozi wa serikali ya wilaya ya Punjob nchini Pakistani wamezuia kufanya maombolezo ya bibi Fatima (a.s) viomgozi ambao wanafuata fikira na mitazamo ya kiwahabi ya Kisaudia, ambapo si maombolezo ya bibi Fatimah tu bali hata maombolezo yote ya vifo vya watakatifu wa madhehebu ya Shia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: viongozi wa wilaya ya Punjab nchini Pakistan wametoa amri mpya ya kuzuia maombolezo yote ya wafuasi wa madhehebu ya Shia, ambapo amri hiyo imetangazwa siku ya kuazimisha maombolezo ya kuuwawa kwa Bibi Zahra binti ya mtukufu mtume Muhammad (s.a.w.w) wilayani humo.
 Amri hiyo imetolewa katika hali ambayo wafuasi wa madhehebu ya Shia walikuwa wamekusanyika kwaajili ya kufanya maombolezo ya kifo cha Bibi Zahra binti ya Mtume (s.a.w.w) katika mji wa Sargodha katika wilaya ya Punjab, ndipo wakakutwa wamezungukwa na majeshi ya Polisi ya wilaya hiyo na kuwakataza kufanya maombolezo hayo.
Waumini hao baada ya kupewa amri hiyo walitaka kujua sababu ya kuzuiliwa kwao kwao kufanya maombolezo hayo ambayo ni moja kati ya haki zao za msingi, ndipo kiongozi wa jeshi hilo alijibu suali hilo na kuonyesha desturi na amri ya viongozi wa wilaya hiyo inayonyesha kukomesha kufanya maombolezo katika welaya nzima ya Punjab nchini Pakistan.
Wafuasi wa madhehebu ya Shia katika wilaya hiyo katika kukabiliana na hukumu wamesisitiza kuwa, hawatakubali kuporwa kwa haki zao za msingi katika kutekeleza ibada na kile wanacho kiamini, kwa kuofia hukumu hiyo, huku wakibainisha kuwa wataendelea kufanya maombolezo ya watakatifu kwa hali yeyote itakayokuwa.
Kiongozi wa mashia katika wilaya ya Punjab ametoa ujumbe mkali katika kukekemea suala hilo, amewataka viongozi wa wilaya hiyo kuacha kufuata wanayoamrishwa na vikundi potovu vya kiwahabi na utawala wa kiwahabi wa Saudi Arabia, badala yake kufuata mwenendo wa Muhammad Ali Jinah (muasisi wa serikali ya Pakistan) katika kuishi na wafuasi wa  madhehebu mengine.
Jambo muhimu kuashiria ni kwamba serikali ya Pakistan inafungamano la karibu na serikali ya Saudi Arabia, iliokuwa na mitazamo potovu ya kiwahabi dhidi ya wafuasi wa madhebu nyingine, ambapo fikra hizo zimepelekea kutokea kufanyika mauaji ya kikatili dhedi wafuasi wa madhehebu ya Shia nchini humo.
mwisho

mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky