Afrika ya kusini imepitisha muswada wa kupunguza fungamano lake na utawala haramu wa Israel

Afrika ya kusini imepitisha muswada wa kupunguza fungamano lake na utawala haramu wa Israel

Chama cha African National Congress cha Afrika ya Kusini katika bunge la Afrika ya kusini kimeafikiana na mpango wa kupunguza fungamano la kidiplomasia na serikali ya kivamizi ya Israel na serikali ya nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikao kilichofanyika chini ya usimamizi wa chama cha African National Congress cha Afrika ya kusini, kimepitisha muswada wa kupunguza fungamano la kidiplomasia la taifa hilo na serikali ya kivamizi ya Israel , ambapo kwa mujibu wa muswada huo seri inapaswa kudhoofisha vungamano lake na serikali ya kivamizi ya Israel kidogokidogo mpaka kufikia kiwango cha chini zaidi.
Mmoja kati ya viongozi wakubwa wa chama hicho katika mahojiano yake na vyombo vya habari vya Afrika ya Kusini nakusema kuwa: kwa mujibu wa muswada huo imependekezwa kuwa, ubalozi wa Afrika ya Kusini mjini Tel Aviv inawajibika kuanza kupunguza vungamano lake na serikali haramu ya kivamizi ya Israel na hatimaye kusitisha uhusiano na taifa hilo la kivamizi.
Aidha kiongozi huyo aliongeza kusema kuwa: kuna baadhi ya viongozi wa baadhi ya majimbo nchini humo wametaka kukata uhusiano kabisa na serikali haramu ya Israel walipokuwa katika mkutano huo nakutaka kufunga ubalozi wa Afrika ya Kusini mjini Tel Aviv haraka iwezekanavyo, ama makubalino ya mwesho katika kikao hicho yameafikiwa kwa pamoja kuwa wanapaswa kupunguza fungamano lao hatua kwa hatua mpaka kufika daraja ya sifuri, huku wakisisitiza kuepuka kufanya haraka katika suala hilo.
Kadhalika amesema: lengo la kupitisha muswada huo ni kutoa ujumbe kukerwa kwao na vitendo vya dhulma vya serikali ya kivamizi ya Israel dhidi ya wananchi wa Palestina hususan suala la kujimilikisha ardhi ya wapalestina na kujenga makazi yao katika sehemu hiyo, huku wakisistiza kutisha kwa haraka kwa vitendo hivyo vya kujenga katika maeneo ya wapalestina na kuwapa haki zao wananchi wa Palestina.
Kiongozi mkuu wa chama cha African National Congress katika bunge la Afrika ya Kusini akisisitiza mwishoni mwa mazungumzo yake kuhusu muswada huo kuwa: kwa masikitiko makubwa ubalozi wetu toka miaka 22 iliopita mpaka sasa haujafanikiwa kufukia malengo ya dharura katika kukabiliana na Israel ili kutatua mgogoro uliopo baina ya Israel na Palestina.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky