Amiri wa Makka: Mahojaji wa Iran ni ndugu zetu katika dini/ matumaini yangu tuwakumbuke kwa wema nao watukumbuke kwa wema

Amiri wa Makka: Mahojaji wa Iran ni ndugu zetu katika dini/ matumaini yangu tuwakumbuke kwa wema nao watukumbuke kwa wema

Amiri mkuu wa mji mtukufu wa Makka amesema: Wairan ni ndugu zetu katika Uislamu nasi tumefurahishwa na kuja kwao katika Ardhi tukufu ya Makka

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na mtoto wa mfalme (Khalid Al-faisal) kiongozi mkuu wa mji mtukufu wa Makka katika kikao cha habari na kuwataja kuwa Wairan ndugu katika dini ya Uilsamu.
Aidha amesema kuwa: mahujaji wa Iran ni ndugu zetu katika dini ambapo tumewapokea vizuri katika ardhi tukufu za Makka.
Amiri wa Makka anaamini ya kwamba Mahujaji wa Iran wameweza kutekeleza ibada ya Hija kwa amani na utulivu na kutopatwa na tatizo la aina yeyote, jambo ambalo litapelekea kuwa ni kumbukumbu njema ya ziara yao nchini Saudi Arabia.
Kiongozi huyo ameonyesha matumaini yake kuwa watakuwa wenye kuwataja Wairan kwa wema, nao Wairan pia watakuwa wenye kuwakumbuka wasudia kwa wema.
Hii ni katika hali ambayo serikali ya Iran ilizuia wananchi wake kwenda kufanya ibada za hija nchini Saudi Arabia, kutokana na kuharibika uhusiano wa nchi hizo mbili, ambapo mwaka huu ndio mwaka wa kwanza kwa Wairan kwenda kufanya ibada ya Hija, baada ya kufanya vikao kadha vya makubaliano baina ya viongozi wa Iran na Saudi Arabia.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky