Ankara: Misri na Israel wazuia kuamisha majeruhi wa Palestina

Ankara: Misri na Israel wazuia kuamisha majeruhi wa Palestina

Uturuki imetangaza kuwa kulikuwa na utaratibu kuwa ndege zozote zinazotaka kuwaamisha majeruhi wa Palistina ni lazima vitumeke viwanja vya ndege vya Misri au Israel, ama mpaka sasa hivi ndege za Uturuki zilioandaliwa kwaajili ya kuchukua majeruhi wa Kipalestina haziruhusiwa kutua katika viwanja vya ndege hivyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: naibu waziri mkuu wa Uturuki amesema: Israel na Misri hawajatoa ruhusa ya kutua ndege za Uturuki katika viwanja vya ndege vyao kwaajili ya kuwahamisha majeruhi wa kipalestina.
Hayo yametangazwa na shirika la habari la Isna kutoka kwa shirika la habari la Anadolu, naibu waziri mkuu wa Uturuki amesema kuwa: kuwasaidia ndugu zetu wanao dhulumiwa Palestina ni wadhifa kwetu kidini.
Aidha ameongeza kusema kuwa: ndege za Uturuki ziliotumwa kwenda kuwachukuwa majeruhi wa Palestina, zimezuiliwa kutua katika viwanja vya ndege vya Misri na Israel, huku akisisitiza kuwa Uturuki itaendelea kuonyesha msimamo wake katika kuwasaidia wapalestina.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky