Ansarullah: makombora yetu yatashambulia sehemu ambayo adui hatarijii kuwa yatafika

Ansarullah: makombora yetu yatashambulia sehemu ambayo adui hatarijii kuwa yatafika

Msemaji mkuu wa kikundi cha Ansarullah nchini Yemen amesisitiza kwa kusema kuwa, kila hujuma zinaposhadidi dhidi yetu na kuendelea kwa vita dhidi ya Yemen, uwezo wetu wa kukabiliana na uvamizi unazidi kukuwa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Muhammad Abdusalam, msemaji mkuu wa kikundi cha Ansarullah nchini Yemen amesisitiza kuwa mashambulizi ya makombora yetu yatafika na kushambulia sehemu ambazo maadui zetu hawatarajii kuwasili katika sehemu hizo, ambapo hayo yote ni juhudi za wanachi wote na umoja wa kitaifa nchini humo.
Aidha maelezo ya Abdusalam yametokea kufuatia mashambulizi yaliofanywa na kikosi cha makombora nchini Yemen kutangaza shambulio waliofanya nchini Saudi Arabia na kutua sehemu iliokusudiwa katika mji wa Riyadh nchini humo.
Naye aliendelea kusema kuwa umoja wa  kivamizi chini ya usimamizi wa Saudi Arabia imetoa rushwa ya Dola milioni 30 kuipatia shirika moja la nchi za kimaghiribi kwaajili ya kuifanya moja kati ya televishen zetu isiwe inapatikana kwa muda wa mwezi mmoja.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky