Asilimia 91 ya ardhi ya Syria amekombolewa kutoka kwa Magaidi

Asilimia 91 ya ardhi ya Syria amekombolewa kutoka kwa Magaidi

Wizara ya ulinzi na usalama ya Urusi imetangaza kuwa ni asilimia chini ya 10 ya ardhi ya Syria ndio ambayo mpaka sasa hazijakombolewa na ziko chini ya magaidi wa Daesh nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya ulinzi ya Urusi imeonyesha ramani ya maeneo yaliokuwa chini ya kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria ambapo inaonyesha kuwa asilimia 91 ya ardhi ya Syria zimeshakombolewa kutoka mikononi mwa magaidi.
Aidha wizara hiyo emeeleza kuwa majeshi ya anga ya Urusi nchini Syria yamerusha ndege za kijeshi nchini humo mara 500 kwa wiki, ambapo kufuatia mashambulio hayo sehemu 1400 za magaidi hao zemesambaratishwa, huku wakiashiria kuwa walifakiwa kufanya hao baada ya kupata ripoti makini znazoashiria maeneo ya mkusanyiko wa magaidi wa kikundi cha Daesh na vikundi vingine nchini Syria.
Wiki iliopita Rais wa Urusi alisema alipokutana na Rais wa Uturuki mjini Ankara kwamba, hali ya sasa nchini Syria inaleta matumani ya kumaliza vita dhidi ya vikundi vya kigaidi, ambapo makao makuu ya jeshi la Urusi linamtazamo huo wa kumaliza vita hivi karibuni kama ilivyokuwa imetoa ahadi hapo awali.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky