Boko Haram ya waachia huru mateka wa kike 82

Boko Haram ya waachia huru mateka wa kike 82

Serikali ya Nigeria imesema wasichana 82 wa waliotekwa nyara na magaidi wa Boko Haram miaka mitatu iliyopita wameachiwa huru na katika makubaliano ya kuwaachia huru wafungwa wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Nigeria imesema wasichana 82 wa waliotekwa nyara na magaidi wa Boko Haram miaka mitatu iliyopita wameachiwa huru na katika makubaliano ya kuwaachia huru wafungwa wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaid la Boko Haram lenye uhusiano na kundi la kigaidi la Daesh.

Ofisi ya Rais imetangaza miezi kadhaa ya mazungumzo na majihadi hao yamezaa matunda miezi sita baada ya wasichana wengine 21 kuachiwa huru na Boko Haram. Hata hivyo hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu idadi ya washukiwa wanachama wa kundi hilo la waasi walioachiwa huru.

Wasichana hao walioachiwa huru watasafirishwa hadi mji mkuu wa Nigeria, Abuja Jumapili ili kukutana na Rais Muhamadu Buhari. Rais Buhari ameishukuru serikali ya Uswisi, Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu na mashirika kadhaa ya kimataifa na ya Nigeria yasiyokuwa ya serikali kwa kusadia katika kuaachiwa huru kwa wasichana hao wa Chibok.

Kuachiwa kwa wasichana wa Chibok kwaibua matumaini

Duru za kijeshi na za kiraia katika mji wa Banki ulioko mpakani kati ya Nigeria na Cameroon zimearifu kuwa takriban wasichana 80 walifikishwa mjini humo Jumamosi adhuhuri na kupelekwa katika kambi za kijeshi.

Seneta wa Nigeria Shehu Sani ambaye alihusika katika mazungumzo ya awali ya kuachiwa huru kwa wasichana hao amesema wengi wao wako katika hali nzuri ya afya. Serikali imesema inafanya kila juhidi kuhakikisha wasichana wengine wa Chibok ambao bado wako mikononi mwa waasi hao wanaachiwa huru.

Boko Haram waliivamia shule ya wasichana ya sekondari katika mji wa Chibok mnamo tarehe 14 Aprili 2014 na kuwateka nyara wasichana 276 waliokuwa wanajiandaa kufanya mitihani yao ya kitaifa. 57 kati yao walifanikiwa kutoroka lakini 219 walizuiwa na kundi hilo.

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau aliyeapa kuwasilimisha na kuwaoza wasichana hao wa Chibok katika kipindi hca nyuma alisema wasichana hao wataachiwa huru iwapo serikali ya Nigeria itawaachia huru wapiganaji wake wanaouzuiwa.

Siku ya Ijumaa, Uingereza na Marekani zilionya kuwa Boko Haram inapanga kuwateka nyara raia wa kigeni katika eneo la Banki, hatua iliyosababisha kusitishwa shughuli ya kupeleka misaada ya kibinadamu katika eneo hilo.

Mwisho wa habari / 291

 

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky