Bunge la Marekani kuchunguza ikiwa Obama aliamuru kudukuliwa kwa simu ya Trump

Bunge la Marekani kuchunguza ikiwa Obama aliamuru kudukuliwa kwa simu ya Trump

Ikulu ya Marekani White House sasa imeliomba bunge kuchunguza ikiwa rais wa zamani Barrack Obama alitumia visivyo mamlaka yake kuamuru kudukuliwa na kuchunguzwa kwa mawasiliano ya simu ya rais wa sasa Donald Trump

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Ikulu ya Marekani White House sasa imeliomba bunge kuchunguza ikiwa rais wa zamani Barrack Obama alitumia visivyo mamlaka yake kuamuru kudukuliwa na kuchunguzwa kwa mawasiliano ya simu ya rais wa sasa Donald Trump wakati wa kampeni za urais mwaka uliopita. White House imetaka uchunguzi huo kuwa miongoni mwa uchunguzi unaoendelea sasa kuhusu uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa mwaka 2016. Ombi hilo limejiri siku moja tu baada ya Rais Trump kudai kuwa Obama aliamuru kudukuliwa kwa mawasiliano ya simu yake iliyoko Trump Tower ambayo ndiyo ilikuwa makao makuu ya kampeni zake. Trump hakutoa ushahidi wa madai yake. Hata hivyo msemaji wa Obama Kevin Lewis alisema madai hayo ni uongo na kuongeza kuwa sheria kuu ya utawala wa Obama ilikuwa ni kutoingilia kati uchunguzi unaofanywa na idara ya sheria ambao unatakiwa ufanyike bila ya kuwepo kwa ushawishi wa kisiasa. Kwa hivyo hakuna afisa yeyote wa ikulu aliyeamuru uchunguzi dhidi ya raia yeyote wa Marekani.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky