Bunge lapitisha mswada kuwa Israel ni nchi ya Kiyahudi

Bunge lapitisha mswada kuwa Israel ni nchi ya Kiyahudi

Bunge la Israel limepitisha sheria inayoielezea Israel kama taifa huru la Wayahudi.
Ikumbukwe kuwa Uyahudi ni dini tofauti na ukristo na uislamu, dini hii inamtambua nabii Musa kuwa ndio mtume wao, haimtambui Yesu wala mtume Muhammad s.a.w.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Bunge la Israel limepitisha sheria inayoielezea Israel kama taifa huru la Wayahudi.

Ikumbukwe kuwa Uyahudi ni dini tofauti na ukristo na uislamu, dini hii inamtambua nabii Musa kuwa ndio mtume wao, haimtambui Yesu wala mtume Muhammad s.a.w.

Baadhi ya wabunge wa Kiarabu walipiga kelele na kuchanachana makaratasi baada ya kura hiyo, na kiongozi wa chama chao Yaman Odeh, amesema katika taarifa kuwa sheria hiyo inachokifanya ni kutoa hadhi ya kisheria kwa utengano na ubaguzi, na kuongeza kuwa hiyo ni sheria ya ubora wa Wayahudi inayowaweka kando zaidi ya asilimia 20 ya raia, ambayo imetengenezwa kukaidi, kugawa na kundeleza uchochezi wa serikali ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu.

Serikali ya Israel inasema sheria hiyo  itaipa tu hadhi ya kisheria hali ya sasa ya Israel. Waziri Mkuu Netanyahu ametetea sheria hiyo na kusema kupitishwa kwake ni hatua muhimu katika kumbukumbu za vuguvugu la uzayuni na historia ya taifa la Israel.

"Tutaendelea kuhakikisha haki za kiraia katika demokrasia ya Israel, haki hizi hazitakiukwa, lakini pia walio wengi wana haki na walio wengi ndio wanaamua. Waliowengi zaidi wanataka kuhakikisha hadhi ya Kiyahudi ya taifa letu kwa vizazi vingi vijavyo," alisema Netanyahu baada ya kura hiyo.

Sheria hiyo ambayo inatajwa kuwa ya kiishara zaidi, imepitishwa muda mchache baada ya nchi hiyo kuadhimisha miaka 70 tangu kuundwa kwa taifa la Israel baada ya kuchukua kwa nguvu ardhi za waarabu. Hatua hii Inaainisha kwamba Israel ndiyo taifa la kihistoria la Wayahudi na wana haki ya kipekee ya uhuru katika taifa hilo.

Hata hivyo Iran imeendelea kusisitiza kuwa haitambui uhalali wa taifa la Israel na kwamba taifa hilo lazima liondolewe katika raman ya dunia.

Sheria ya ubaguzi na utengano

Pia sheria hiyo imeiondolea lugha ya Kirabu hadhi yake kama lugha rasmi sambamba na Kiebrania, na kuishusha kuwa "hadhi maalumu" inayoiwezesha kuendelea kutumika katika taasisi za nchini humo.

Waislamu wa Israel wanafikia milioni 1.8, sawa na karibu asilimia 20 ya idadi jumla ya wakaazi milioni 9. Rasimu za awali za sheria hiyo zilikwenda mbali katika kile wakosoaji ndani na nje waliona kama ubaguzi dhidi ya raia wa Kiarabu, ambalo kwamuda mrefu wamelalamika kuchukuliwa kama raia wa daraja la pili.

Vipengelee kadhaa vilivyoondolewa katika dakika za mwisho kufuatia upinzani wa rais wa Israel na mwanasheria mkuu, vingejumlisha kuanzishwa kwa jamii za Wayahudi pekee, na kuziangiza mahakama kuhukumu kwa mujibu wa sharia za Kiyahudi panapokuwa hakuna hukumu ya mfano katika suala husika.

Lakini hata baada ya mabadiliko, wakosoaji wamesemasheria hiyo mpya itaongeza hisia za kutengwa miongoni mwa jamii za Waislamu walio wachache.

"Muswada wa sheria ya utaifa ni uhalifu wa chuki, wanawabagua kabisaa raia wa kiislamu, dhidi ya Waarabu wachache, ina ibara za kibaguzi, hasa zinazohusu makaazi ya Wayahudi, na zile zinazoshusha hadhi ya lugha ya Kiarabu," alisema Ahmed Tibi, mbunge wa chama cha Waarabu katika bunge la Knesset.

Jamii ya Waarabu wa Israel inahusisha hasa wazawa wa Wapalestina waliobakia kwenye ardhi yao wakati wa mgogoro kati ya Waislamu ya Wayahudi ambapo  mayahudi walichukua kwa nguvu ardhi za waarabu na kusababisha vita vya mwaka 1948, vilivyopelekea kuundwa kwa taifa la sasa la Israel. Mamia kwa maelfu  ya wapalestina walilaazimika kuyaacha makaazi yao au kukimbia.

Mwisho wa habari / 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky