CIA yaituhumu Iran kumsaidia Osama

CIA yaituhumu Iran kumsaidia Osama

baada ya maafisa wa Iran kutaka kutoa ushahidi wa mahusiano ya Marekani na makundi ya kigaidi, ambayo inayapa msaada kushambulia Syria na Iraq pia msaada wa Marekani kwa Al-qaida wakati wa vita vya Urusi, kumepelekea Marekani kufuta haraka habari hizi mtandaoni.
Ukweli ni kwamba Iran imekuwa mstari wa mbele kuzisaidia nchi za jirani kupambana na magaidi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: CIA imechapisha nyaraka zinazodaiwa kupatikana katika operesheni ya kumkamata kiongozi wa al Qaida, Osama bin Laden, mwaka 2011. CIA imedai kuwa Nyaraka hizo zimeibua maswali kuhusu Iran kuunga mkono kundi hilo la kigaidi.

Maafisa wa kijasusi wa Marekani pamoja na waendesha mashtaka kwa muda mrefu wamekuwa wakisema kwamba Iran tangu mwaka 1991 imekuwa na uhusiano na kundi la al Qaida ambalo linamilikiwa na raia wa Saudia arabia. Hiyo ni  moja ya taarifa zilizopatikana katika ripoti ya kurasa 19 iliyoandikwa kwa lugha ya Kiarabu na ambayo ni sehemu ya nyaraka 47,000 zilizochapishwa na CIA.

Iran kwa upande wake daima imekuwa ikikanusha uhusiano wowote na makundi ya kigaidi likiwemo al Qaida na imekuwa ikipambana na makundi hayo. Hata hivyo, ripoti iliyochapishwa na CIA inaonyesha namna ambavyo bin Laden, aliyekuwa mtu mwenye itikadi kali za Kisunni wahabia na aliyetokea Saudi Arabia, nchi ambayo ni makao makuu ya waislamu wa misimamo mikali, CIA inadai kuwa Osama aliweza kuvuka mgawanyo wa kimadhehebu na kutafuta mshirika kwa Wairan wa Kishia, kwa lengo la kumlenga adui yao wa pamoja ambaye ni Marekani.

Ripoti inaeleza Iran iko tayari kumsaidia mtu yeyote anayetaka kuipiga Marekani. Shirika la habari la Marekani, AP, lilipatiwa nakala ya ripoti na nyaraka nyingine zilizokamatwa na CIA. Miongoni mwa mambo mengine, zinajumuisha pia video za harusi ya mtoto wa bin Laden, Hamza. Video hizo hazijawahi kuonyeshwa hadharani na ni mara ya kwanza kwa Hamza kuonekana akiwa mtu mzima. kabla ya hapo, picha na video zilizokuwa zimesambaa zilimwonyesha akiwa bado mtoto. Inaaminika kuwa Hamza bin Laden anaandaliwa kuwa kiongozi mpya wa al Qaida.

Iran yakanusha madai ya kitoto ya CIA

CIA awali iliweka nyaraka za al Qaida mtandaoni lakini baadaye ikaziondoa, ikisema pamekuwa na hitilafu za kiufundi. Nyaraka hizo zinaelezea kile kinachoaminiwa kuwa historia ya uhisiano baina ya al Qaida na Iran. Inaonyesha kwamba Iran ilijitolea kuipa al Qaida fedha, silaha na kingine chochote ambacho kundi hilo lingehitaji. Iran pia ilikuwa tayari kuwapa magaidi mafunzo katika kambi za kundi la Hezbollah nchini Lebanon. Al Qaida kwa upande wake ilitakiwa kushambulia mali na miundombinu ya Wamarekani nchini Saudi Arabia ambapo Saudia ndio mdhamin mkuu wa kundi hilo.

Taarifa hiyo inaendana na ripoti ya serikali ya Marekani iliyoandikwa na kamisheni ya kupeleleza mashambulio ya kigaidi ya World Trade Center na Pentagon mwaka 2001. Ripoti hiyo inasema maafisa wa Iran walikutana na viongozi wa al Qaida nchini Sudan mwaka 1991 ama 1992. Kamisheni hiyo ileleza pia kuwa wanamgambo wa al Qaida baadaye pia walipatiwa mafunzo Lebanonon kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Kishia, Hezbollah. Mpaka leo hii, Iran inaiunga mkono Hezbollah.

Hata hivyo, serikali ya Iran imekanusha madai hayo ya kitoto, ambapo inasadikiwa baada ya maafisa wa Iran kutaka kutoa ushahidi wa mahusiano ya Marekani na makundi ya kigaidi, ambayo inayapa msaada kushambulia Syria na Iraq pia msaada wa Marekani kwa Al-qaida wakati wa vita vya Urusi, kumepelekea Marekani kufuta haraka habari hizi mtandaoni.

Ukweli ni kwamba Iran imekuwa mstari wa mbele kuzisaidia nchi za jirani kupambana na magaidi.

Mwisho wa habari / 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky