Daesh inalengo la kuunda serikali ya kigaidi mashariki ya Asia

Daesh inalengo la kuunda serikali ya kigaidi mashariki ya Asia

Waziri wa ulinzi wa Malaysia ametangaza kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh kinapanga mpango wa kutaka kutengeza utawala wa kikundi hicho nchini mashariki mwa Asia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri wa usalama wa Malaysia ametangaza kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh kinafanya juhudi kubwa ya kutaka kutengeza serikali ya Ukhalifa wa kigaidi mashariki wa bara la Asia.
Hayo yamesemwa na Hishamu dini Husein kuwa serikali ya Philippines, Malaysia na Indonesia, hivi sasa inapambana vikali na kikundi cha kigaidi cha Daesh, na kusini mwa mashariki mwa Asia na mashariki mwa Philippines ndizo sehemu za kuanzia kwa harakati za kigaidi katika maeneo hayo.
Aidha waziri hiyo ameongeza kusema kuwa: kikundi cha kigaidi cha Daesh kina lengo la kuasisi tawi la serikali ya kikundi hicho cha kigaidi katika maeneo ya kusini mwa bara la Asia chini usimamizi wa Abubakari Al-baghdadiy.
Inasemekana kwamba kikundi cha kigaidi cha Daesh baada ya kushindwa nchini Iraq na Syria, kina fanya juhudi za makusudi za kuasisi kutengeza ngome mpya katika baadhi ya mataifa mengine ya bala la Asia kwa katika mataifa ambayo wanapatikana kwa wengi wafuasi wa madhihebu ya kigaidi ya kiwahabi (masalafi) .
Kwa mujibu wa maelezo ya wahariri ni kwamba ni zaidi ya taasisi 30 za kikundi cha kigaidi cha Daesh ziaendesha harakati zake nchini Philippines, Bangladesh, Malaysia na Indonesia.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky