Daesh waitishia kufanya vitendo vya kigaidi katika taifa la China

Daesh waitishia kufanya vitendo vya kigaidi katika taifa la China

Kikundi cha kigaidi cha Daesh chaitisha serikali ya China kuwa hivi karibuni watafanya vitendo vya kigaidi nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha kigaidi cha Daesh kimesambaza video nchini Iraq ambayo inatishia amani ya taifa la China na wananchi wake.
Katika video hiyo ya kikundi hicho cha kigaidi, gaidi mmoja ambaye ni mwananchi wa China anaonekana akikata kichwa cha mtu mmoja aliokuwa na tuhuma ya ujasusi, ambapo gaidi huyo baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama alisema kwa lugha ya kichina kuwa; sisi ni wanajeshi wa Daesh tuko njiani kuja China ambapo tutakuja kumwaga damu zeno kwaajili ya kulipa kisasi cha waislamu nchini humo.
Video hiyo imeonyesha mafunzo wanayopewa magaidi wa China na watoto zao, ikiwemo mafunzo ya ukatili ya kuuwa watu wasiokuwa na hatia.
Serikali ya China mara kadhaa ilieleza kuwa vikundi vya kigaidi viliopo nje ya China vinamalengo ya kufanya mashambulio ya kigaidi katika maeneo yanayokaliwa na Waislamu ya Xinjiang nchini humo.
Wizara ya ulinzi ya China imetangaza kuwa mnamo mwaka 2015 watu miamoja ambao ni wananchi wa nchi hiyo wamekwenda nchini Uturuki, Iraq na Syria kwaajili ya kujiunga na vikundi vya kigaidi hususan kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria.
Aidha hapo mwanzo balozi wa Syria nchini China alitangaza kuwa: wananchi elfu tano wa China wamejiunga na vikundi vya kigaidi nchini Syria ambao kwa sasa wanakabiliana na majeshi ya Syria nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky