Daesh washambulia tena katika Ardhi ya Libanon

Daesh washambulia tena katika Ardhi ya Libanon

Kikundi cha kigaidi cha Daesh chashambulia kwa makombora saba nchini Lebanon

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kwa mujibu wa ripoti ziliotufikia hivi punde ni kwamba kikundi cha kigaidi cha Daesh chaendelea kufanya mauaji nchini Lebanon.

kikundi cha kigaidi cha Daesh siku ya jumatatu kimeshambulia kwa makombora saba katika ardhi ya Lebanon, ambapo makombora hayo yalishuka pembezoni mwa mji wa “Alqaa”, huku ikielezwa kuwa shambulio hilo halijasababisha maafa ya mtu kupoteza maisha.

Majeshi ya Lebanon katika kujibu mashambulio hayo, yameshambulia maeneo ya kikundi hicho cha kigaidi cha Daesh nchini humo.

Kikundi cha kigaidi cha Daesh kinamiliki maeneo machache yaliopo katika mipaka ya Syria na Lebanon, ambapo magaidi hao daima hushambuliana na majeshi ya nchi hiyo na majeshi ya kikundi cha Hizbullah nchini humo.

Wapiganaji wa kikundi cha Hizbullah katika masiku ya hivi mwishoni, wamefanikiwa kuikomboa sehemu ya Jurudul Arsal ndani ya ardhi ya Lebanon nakuwasambaratisha magaidi hao katika sehemu hiyo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky