Daesh watangaza makao makuu mapya ya mji wa Tal Afar baada ya mji wa Musol

Daesh watangaza makao makuu mapya ya mji wa Tal Afar baada ya mji wa Musol

Kikundi cha kigaidi cha Daesh baada ya kushindwa kuumiliki mji wa Musol, sasa watangaza mji wa Tal Afar kuwa ndio makao makuu ya kikundi hicho nchini Iraq, huku wakisistiza kuwa huduma zote za serikali ya kikundi hicho yatafanywa katika mji huo wa wa Tal Afar

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: chanzo kimoja cha Habari katika mkoa wa Neneveh ametangaza kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh baada ya kushindwa katika mji wa Musol, wamechagua mji wa Tal Afar kuwa ndio utakaoshika nafasi ya mji wa Musol kwa mujibu wa kikundi hicho.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh kimetoa kauli katika mji wa Tal Afar ndio seduhemu ya kuwahudumia magaidi wa kikundi hicho katika huduma zote za kijamii ya kikundi hicho cha kigaidi.
Kutangazwa kwa mji huo kuwa ni makao makuu ya kikundi cha kigaidi cha Daesh baada ya mji wa Musol ni alama ya kukubali kushindwa kwa kikundi hicho katika mji wa Musol, hivyo kulazimika kuanisha sehemu ya pili itakayoshika nafasi ya Musol.
Inasemekana kuwa kikundicha kigaidi cha Daesh mwezi juni mwaka 2014 waliutangaza mji wa Musol uliopo katika mkoa wa Neneveh kuwa ndio makao makuu ya utawala wa kigaidi wa Daesh na baada ya hapo walifanikiwa kuziteka sehemu nyingine mbalimbali za mikoa ya Iraq.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky