Emirates baada ya Saudi Arabia, Bahrain na Kuwait yawataka wananchi waondoke haraka Lebanon

Emirates baada ya Saudi Arabia, Bahrain na Kuwait yawataka wananchi waondoke haraka Lebanon

Nchi ya Saudi Arabia, Kuwait, Emirates na Bahrain zawataka wananchi wao wanaoishi nchini Lebanon kurudi nchini kwao haraka iwezekanavyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: serikali ya umoja wa Falme za Kiarabu (Emirates) baada ya serikali ya Saudi Arabia, Bahrain na Kuwait, imewataka wananchi wake wanaoishi nchini Lebanon kuondoka nchini humo, kwa kile kilichodai serikali hiyo, hali ya Lebanon haipo vizuri kiusalama kwa sasa.
Kabla ya hapo pia serikali ya Saudi Arabia na Bahrain zilikuwa zimeshatoa kauli zinazofana zinazowataka wananchi wa mataifa hayo kurudi nchini kwao haraka iwezekanavyo.
Siku ya Jumamosi “Saad Hariri” waziri mkuu wa Lebanon akiwa amesafiri nchini Saudi Arabia alitangaza kujiuzuru nafasi yake ya uwaziri mkuu. Baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza kuwa kujiuzuru kwa Saad Hariri kumetokea baada ya serikali ya Saudi Arabia kumlazimisha kufanya hivyo, kwalingo la kuleta shinikizo kwa serikali ya Lebanon na kuleta sintofahamu nchini humo.
Wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia baada ya siku moja ya kujiuzulu Hariri ilitangaza kuwa Baraza la Mawaziri la Lebanon, ni Baraza la uadui kutokana na kushiriki Hizbullah katika baraza hilo.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky