Gaidi wa kujiripua wa Daesh aamizwa katika mji wa Tikrit nchini Iraq

Gaidi wa kujiripua wa Daesh aamizwa katika mji wa Tikrit nchini Iraq

Gaidi mmoja aangamizwa katikati ya soko ambapo alikuwa anataka kufanya shambulio la kujiripua katika mji wa Tikrit Kaskazini mwa Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jeshi la wananchi la kujitolea nchini Iraq limefanikiwa kumsambaratisha gaidi mmoja aliokuwa analengo la kujiripua nchini Iraq, ambapo walifanikiwa kumsabaratisha kabla ya kufanya jaribio lake hilo.
Jeshi hilo lilifanikiwa kufanya hivyo siku ya Jumamosi ambapo gaidi huyo alikuwa amepanga kujiripua katikati ya soko liliopo katika mji wa Tikrit mji ambao upo kaskazini mwa Iraq, ambapo gaidi huyo alikusudia kujiripua katika mjumuiko mkubwa wa raia wasiokuwa na hatia nchini humo.
Majeshi ya wananchi waliokuwa wamejitolea baada ya kukamilisha kusambaratisha jaribio hilo, limepanga mpango mkali wa kukabiliana na vitendo vya kigaidi katika sehemu hiyo huku wakishadidisha ulinzi na dolia katika mji wa Tikrit.
Mpaka sasa jeshi hilo ni miaka miwili toka wafanikiwe kuukomboa mji wa Tikrit kutoka mikononi mwa magaidi wa kikundi cha Daesh nchini humo.
Waziri mkuu wa Iraq mwezi mmoja uliopita alitangaza kukombolewa mji wa Musol kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo kiliufanya mji huo kuwa ni makao makuu ya serikali yao ya ugaidi nchini Iraq.
Majeshi ya Iraq nayo yamejipanga ipasavyo kwaajili ya kuanza mapambano ya kuukomboa mji wa Tal Afar kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh, mji ambao uko katika mkoa wa Nineveh kaskazini mwa Iraq ambapo ipo karibu na mji wa Musol.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky