Hatimaye Zakzaky aruhusiwa kufanyiwa vipimo+ picha

Hatimaye Zakzaky aruhusiwa kufanyiwa vipimo+ picha

Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye miaka miwili jela leo aruhusiwa kuhojiwa na vyombo vya habari baada ya kumaliza kufanyiwa vipimo katika hospitali za nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Sheikh Ibrahim kiongozi mkuu wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria ambaye ni miaka miwili aliwekwa ndani kinyume na Sheria, leo siku ya Jumamosi alionekana baina ya waandishi wa habari.
Naye baada ya kumaliza kufanyiwa vipimo katika Hospitali moja iliopo mjini Abuja alipata ruhusa ya kuongea na waandishi wa habari, Sheikh Zakzaky alisema kuwaambia waandishi wa Habari kwamba: mimi bado niko hai na nimewa ruhusa ya kufanyiwa vipimo na Daktari wangu, aidha katika mahojiano hayo mafupi amewashukuru wananchi wa Nigeria kwa kumuahami kwao.
Ruhusu hiyo amepewa baada ya vyombo vya habari kusambaza kwa habari za maandamano yaliokuwa yanaitaka serikali kumuacha huru Sheikh Zakzaky kutokana na hali mbaya ya afya aliokuwa nayo, maandamo ambayo yalivamiwa na jeshi la Polisi na kusababisha kujeruhiwa kwa baadhi ya watu na mmoja kuteza maisha nchini humo.


mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky