Hizi ndio sababu ya Chuki za baina ya Saudi Arabia na Iran

Hizi ndio sababu ya Chuki za baina ya   Saudi Arabia na Iran

Ifahamike kwamba wairan si waarabu ni waajemi, hivyo Saudia arabia inaungwa mkono na takriban nchi zote za kiarabu na Marekani kuwa dhidi ya Iran.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Uhusiano baina ya taifa mawili yenye kungu na ushawishi mkubwa la Mashariki ya kati, Saudi Arabia na Iran,  kwa miongo mingi umekuwa wa wasiwasi kutokana na nchi hizo kuzozana kuhusu masuala matatu dini, mali, na utawala.

Kila mmoja anajinasibu kuwa mtetezi wa  madhehebu mawili makuu ya dini ya kiislamu. Saudi Arabia, inatetea dhehebu la Sunni wahabia na Iran ipo upande wa dhehebu la Shia.

 Hayo yanajiri wakati mvutano huo ukiongezeka wiki hii, baada ya Riyadh kuituhumu Tehran kwa  kufanya uvamizi wa kijeshi wa moja kwa moja unaohusishwa na vita vya Yemen, ambapo wapiganaji wa Yemen ambao wamekuwa wakiangamizwa na makombora ya Saudia arabia na washirika wake, wamefanya mashambulizi makali nchini  Saudia arabia.

 Sababu kuu za mivutano baina ya nchi hizo mbili

Ifahamike kwamba wairan si waarabu ni waajemi, hivyo Saudia arabia inaungwa mkono na takriban nchi zote za kiarabu na Marekani kuwa dhidi ya Iran.

Mwaka 1973 wakati wa vita vya waarab na Israel ambapo waarabu walipigwa vibaya, na hatimaye umoja wa waarabu kudhoofika na kuona kuwa Israel ni taifa lisilopigika.

Jamhuri ya kiislamu ya Iran, ilianzishwa Aprili 1979 baada ya mapinduzi yaliyouondoa utawala wa kifalme wa Shah ulioelemea nchi za magharibi. mataifa  ya kiarabu katika kanda hiyo yakaishutumu  Iran kuwa inataka kuendeleza mapinduzi yake katika nchi hizo.

Mnamo Septemba 1980, Saddam Hussein akisaidiwa na Marekani aliivamia Iran na kusababisha vita vilivyodumu kwa miaka nane. Saudi Arabia, na mataifa ya kiarabu yalliisaidia kifedha serikali ya Iraq dhidi ya Iran, na kuzishawishi nchini nyingine zenye waumini wengi wa madhehebu ya  Sunni, kufanya hivyo hivyo. Na kusambaza fikra mbovu kuwa Iran ni mashia na Mashia ni makafiri hivyo waislamu wanatakiwa kuipiga Iran.

Askari wa usalama wa Saudi waliwaua mamia ya waandamanaji wa mahujaji wa kiirani katika maandamano  ya amani ya wairan ya kupinga dhuluma za Marekani  mjini Mecca Julai 1987 . Zaidi ya watu 600 wengi wakiwa raia wa Iran, waliuawa, huku serikali ya Saudia arabia ikijifaharisha kwa mauaji hayo.

Kufuatia mauaji hayo Raia wa Iran wenye hasira waliuvamia na kupora mali katika ubalozi wa  Saudi, mjini Tehran,  Saudi Arabia ikavunja uhusiano wa kibalozi  na Iran.

Uvamizi wa Iraq, ulioongozwa na Marekani mwaka 2003 kwa lengo la kumtoa madarakani kibaraka wao Saddam Husein, ulizusha mzozo mpya kwa kukiondoa chama Baath,  kilichokuwa kikitawala na hatimaye mashia waliwashinda wamarekani na kushika hatamu za uongozi wa Iraq. Hatua hiyo  ilisababisha Iraq kuwa chini ya ushawishi wa Iran ambayo pia iliwasaidia katika kuwatoa wamarekani nchini humo. 

Wakati maandamano yakichipuka katika nchi za Mashariki ya Kati mwaka 2011, Saudia arabia iliyatuma majeshi yake kwa nchi jirani ya Bahrain ili kuzima maandamano na nguvu za mashia ambazo zimekuwa tishio na hatimaye kuwaua na kujerehi mamia ya wananchi, ambapo mpaka hivi sasa nchi hiyo haina utulivu

Saudia arabia  iliishutumu Iran kwa kuchochea  mzozo  huo katika visiwa vya Bahrain vinavotawaliwa na  Wasuni ingawa wananchi wengi ni wadhehebu la shia.

Mahasimu hao walijiandaa tena kwa mapigano mapya,  mwaka 2011, wakati mzozo wa Syria ulipozuka.

Iran ilimsaidia Rais Bashar al-Assad kwa kumpa vikosi vya kijeshi na fedha ili kupambana na magaidi wa dhehebu la Sunii ambao wanaungwa mkono na Saudia arabia na washirika wake kwa lengo la kumtoa madarakani rais wa Syria.

Magaidi hao waliojiita Dola la kiislamu waliingia mpaka Iraq na kuwaua maelfu ya waislamu wa dhehebu la Shia, ambapo Iran ilituma majeshi yake Iraq na Syria na kupambana na magaidi hao kwanzia mwaka 2011 mpaka leo, na hatimaye magaidi wanaoungwa mkono na Saudia arabia ikisaidiwa na Marekani na nchi za magharibi wanaelekea kushindwa vita hivyo, na kuipa ushindi mkubwa Iran.

Kadhalika, Saudi Arabia na Iran, wanapingana kuhusu Yemen. Machi 2015 Riyadh iliunda muungano wa waarabu wa Sunni, na kufanya mashambulizi makali dhidi ya wananchi wa Yemen kwa lengo la kumrudisha rais wa Yemen ambaye wananchi hawamtaki, wakati Tehran ikiwasaidia wananchi wa Yemen na wanamgambo wa Huthi wa dhehebu la Shia katika kupambana na mataifa 11 yanayoongozwa na Saudia arabia katika mashambulizi hayo. Lakini mpaka sasa majeshi ya Saudia arabia na washirika wake yameshindwa hata kuteka mji mmoja wa Yemen na badala yake wananchi wa Yemen wakiungwa mkono na Iran wameteka miji miwili ya Saudia arabia na kurusha makombora mpaka Riyadh mji mkuu wa  Saudia arabia.

Mnamo mwaka 2015 askari wa Saudia arabia waliwateka vijana wawili wa kikume wa Iran waliokwenda kuhiji na kulawiti, jambo lililoichukiza Iran kwa hali ya juu.

Mnamo Septemba 2015, mahujaji zaidi ya 4000 wakiwamo mamia ya Wairan, walipoteza maisha kutokana na kukanyagana wakati wa kutekeleza ibada ya hija baada ya barabara kufungwa ili mtoto wa mfalme apite na kusababisha watu kubanana katika njia moja na hatimaye kukanyagana na kupelekea maelfu ya waislam kupoteza maisha.

Baada ya tukio hilo, kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, alisema viongozi wa  Saudi, hawana uwezo na sifa ya kusimamia hija .

Mnamo Januari 2016, Saudi Arabia, ilimnyonga kiongozi  maarufu wa madhehebu la Washia, sheikh Nimr al-Nimr kwa kosa la kuikosoa serikali ya kifalme.

 Iran ilichukizwa na kitendo hicho na kuita kuwa ni ukatili dhidi ya viongozi wa kidini na hatimaye wananchi wa Iran walivamia ubarozi wa Saudia arabia na kuvunja vunja vitu, na hatimaye Saudia arabia ilizishawishi nchi za kiarabu kuvunja uhusinao na Iran.

Kadhalika Saudia arabia na washirika wake waliamua kuwaita magaidi wanamgambo wenye nguvu wa Hezbollah wa madhehebu ya Shia nchini Lebanon, ambao ni washirika wa Iran, ambao pia kwa mara ya kwanza jeshi lao liliishinda Israel katika vita vya mwaka 2006, jambo lililoudhi umoja wa waarabu kwani walijikusanya nchi zaidi ya tano kuipiga Israel wakashindwa lakini kikundi kidogo cha wanamgambo kinachodhaniwa na Iran kimeishinda Israel.

  Mnamo Juni 2017, Saudi Arabia, na washirika wake, walivunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Qatar, baada ya nchi hiyo kutangaza kuwa haioni haja ya kuitenga Iran kwani Iran haina uadui na waarabu.

Baadaye, Oktoba 2017, Saudi Arabia, ilisema inamuunga mkono Rais wa Marekani, Donald Trump na Israel,  katika mikakati yake  madhubuti dhidi ya Iran baada ya kukataa kuthibitisha makubaliano juu ya mpango wa nyuklia wa wa Iran  yaliofikiwa 2015 kati ya Iran na madola sita yenye nguvu duniani ambapo yanaruhusu Iran kukuwa zaidi kiuchumi.

Wakati hayo yakijiri, Novemba 2017, Waziri Mkuu wa  Lebanon, Saad Hariri, alishawishiwa na Saudia arabia na hatimaye kutangaza kujiuzulu akiwa Riyadh,  akidai kuwa kuna njama zinazofanywa na Iran, nchini humo dhidi ya usalama wake, kupitia kundi la Hezbollah.

Hizi ni sehemu muhimu za migogoro kati ya Saudia arabia na Iran.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky