Hospitali yasambaratishwa na majeshi ya anga ya Saudi Arabia

Hospitali yasambaratishwa na majeshi ya anga ya Saudi Arabia

Umoja wa kuivamia Yemen chini ya usimamizi wa serikali ya Saudi Arabia umeshambulia Hospitali moja iliokuwa katika mkoa wa Al-hudaydah

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya afya nchini Yemen imetangaza kuwa majeshi ya kivamizi nchini humo yanayosimamiwa na Saudi Arabia, wameshambulia Hospitali ya “Deraihimi” iliokuwa katika mkoa wa Al-hudaydah magharibi mwa Yemen na kuiharibu Hospitali hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hii, wizara ya afya ya Yeme n katika kauli na ujumbe wake imesema kuwa, umoja wa kivamizi wa Saudi Arabia katika mashambulio yake ya Anga waliofanya mji wa Deraihimi na kupelekea kusambaratika kwa Hospitali kuu ya mji huo.
Kwa mujibu wa ripoti hii mpaka sasa idadi ya waliofariki kufuatia shambulio hilo bado haijafahamika, ambapo kwa upande mwengine magari ya kubebea wagunjwa na nyumba ziliopo karibu na Hospitali hiyo nazo zimeharibika.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky