Husni Mubarak ataachiwa huru Muda si mrefu

Husni Mubarak ataachiwa huru Muda si mrefu

Mahakama kuu ya Misri imeafiki kuachwa huru kwa Husni Mubarak rais wa zamani ya jamhuri ya Misri

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mahakama kuu ya Misri siku ya Jumatau imeafiki kuachwa huru kwa Rais wa zamani wa Misri Husni Mubaraka, ambapo mahakama hiyo ilifikia hukumu hiyo katika kikao kilichofanyika wiki mbili ziliopita, baada ya kufutiwa tuhumu aliokuwa nazo rais huyo msitafu.
“Farid Aldib” ambaye ni wakili wa Rais huyo amesema: mahakama hiyo imeafiki kuachwa huru kwa Husni Mubarak, ambapo baada ya kuruhusiwa na waganga wake, ataweza kutoka kwa masaa kadhaa yajayo kwenda katika familia yake.
Mahakama hiyo mnamo tarehe mbili mwezi Machi mwaka huu, zilifuta tuhuma alizokuwa akituhumiwa Husni Mubara za kushiriki kuuwa wapinzani waliokuwa katika maandamo dhidi ya Rais huyo katika kipindi cha Utawala wake mwaka 2011 nchini humo.
Mahakama kuu ya nchi hiyo katika kutoa hukumu mpya ya tuhumu za Rais huyo wa zamani wa nchi hiyo imetangaza kuwa, Rais wa zamani wa Misr hakushiriki katika mauaji ya waandamanaji waliokuwa wameandamana dhidi yake, maandamano ambayo yalipelekea rais huyo kuenguliwa katika nafasi ya uraisi.
Wakili wa Rais huyo amesema kuwa: mimi nadhani kuwa Mubaraka ataruhusiwa Hospitali hatimaye kwenda nymbani kwake baada ya siku moja au mbili.
mwesho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky