Idadi ya Mayahudi wanaondoka katika Ardhi ya Wapalestina yazidi katika ardhi za Quds

Idadi ya Mayahudi wanaondoka katika Ardhi ya Wapalestina yazidi katika ardhi za Quds

Ripoti mpya kutoka katika Ardhi zinazokaliwa kwa mabavu nchini Palestina, zinaeleza kuongezeka kwa Mayahudi wanaondoka na kuto rudi katika sehemu hizo zinazokaliwa kinyume na sheria nchini Palestina

Shirik la habari AhluBayt (a.s) ABNA: habari hiyo imesambazwa na moja kati ya vituo makini vya hesabu ya watu na makazi cha serikali haramu unakalia kwa mabavu Ardhi za Quds kuwa kunaongezeko kubwa la kuto rudi Mayahudi wanaondoka katika Ardhi hizo, jambo ambalo linaashiria waingie katika mshangao mkubwa nchini humo.
Kituo cha sensa ya watu na makazi katika serikali ya kivamizi ya Israel katika ripoti yake hivi karibuni imetangaza kuwa: kati ya Mayahudi elfu 16 na 700 waliokuwa wameondoka katika sehemu zinazokaliwa kwa mabavu ambapo waliorudi ni Mayahudi 8500 tu, kiwango ambacho kinaonyesha ongezeko ukilinganisha na mwaka 2015 mara dufu.
Hali hiyo inaashiria ongozeko kuondoka kwa Mayahudi hao katika maeneo ya Palestina, ama jambo muhimu linalopaswa kuashiriwa  ni kwamba, jambo hilo limesababshwa na taasisi za kupambana na haki za binadamu na jumuia ya umoja wa Mataifa ambapo mara kwa mara limekuwa likikemea vitendo vya utawala haramu wa Israel ya kuharibu makazi ya Wapalestina na kujenga makazi yaliokuwa kinyume na sheria nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky