Idadi ya walopata maafa ya shambulio la kigaidi nchini Misri,305 wameuwawa 128 majeruhi

Idadi ya walopata maafa ya shambulio la kigaidi nchini Misri,305 wameuwawa 128 majeruhi

Vyombo vya habari nchini Misri yatangaza idadi ya waliopatwa na maafa katika shambulio la kigaidi liliofanywa katika msikiti mmoja kwatika jangwa la Sinai nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: serikali ya Misri yatoa takwimu kamili ya waliopata maafa katika tukio la kigaidi liliotokea jana nchini katika msikiti wa Ar-rawdha nchini humo.
Katika shambulio hilo liliofanywa siku ya Ijumaa lilikuwa katika sura hii kwamba watu waliokuwa na silaha ambao hawakuwa wamefahamika walisahmbulia waumini waliokuwa katika msikiti huo na kusababisha kutokea kwa mauaji ya watu 305 ambapo kati yao 27 ni watoto huku vyanzo hivyo vikiripoti kuwa watu 128 pia wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Msikiti wa Ar-rawdha upo katika mji wa Ar-Rawdha katika mkoa wa Sinai kaskazini mwa nchi hiyo, ambapo magidi 25 waliokuwa wamebeba bendara ya kikundi cha kigaidi cha Daesh kipindi ambacho Imamu wa Sala ya Ijumaa ikitoa hutuba ya sala ya Ijumaa ndipo wakaanza kuwarushia risasi waumini waliopo ndani ya msikiti huo.
Magaidi hao walikuwa na magairi matano na baada ya kufanya shambulio hilo walichuma moto magari 7 ya waumini waliokuwa msikitini, tukio hilo linazingatiwa ni tukio kubwa zaidi liliotokea toka Rais Muhammad Mursiy kupinduliwa nchini humo.
Mkoa wa Sinai upande wa kaskazini kumeanza harakati za kigaidi. Magaidi ambao wako chini ya kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo mpaka sasa mara kadhaa walishakuwa wameyashambulia majeshi ya serikali ya Misri katika sehemu hiyo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky