Imamu wa Ijumaa porwa uimamu nchini Morocco baada ya kutabili kuisha kwa utawala wa Saudia

Imamu wa Ijumaa porwa uimamu nchini Morocco baada ya kutabili kuisha kwa utawala wa Saudia

Wizara ya masuala ya Dini na Waqfu nchini Morocco imemvua cheo cha Uimamu wa sala ya Ijumaa katika mji wa Borkan kwa kosa la kusema kuwa kufunuka kwa pazia ya Kaaba ni ishara ya kuisha utawala wa Saudi Arabia

Shirika la habari AhluLbayt (a.s) ABNA: wizara ya masuala ya dini na Waqfu nchini Morocco imemsimamisha kuendelea kusalisha sala ya Ijumaa Imamu mmoja nchini humo  kwa sababu ya kukosoa mwenendo mbaya wa serikali ya Saudi Arabia.
Wizara hiyo imetangaza siku ya Jumamosi imetangaza  kuwa “Abdulhamid Najariy” kwa sababu ya kukosoa utawala wa Saudi Arabia ambapo alisema mnamo tarehe 20 mwezi wa nane katika hutuba yake iliotoa katika mji wa Borkan.
Kwa mujibu wa video iliosambazwa katika mitandao ya kijamii ni kwamba ilisema tukio liliotokea la kufunuka kwa pazia la Kaaba ni ishara ya kusambaratika utawala wa Saudi Arabia.
Aidha amesema kuwa kufunuka kwa paia ya Kaaba ni tukio ambalo lilitokea katika Ukhalifa wa Bani Abbasi ulipokuwa umekithirisha dhuluma na batili dhidi ya ubinadamu, ambapo baada ya tukio hilo utawala huo ulisambaratika.
Hivyo basi aliesema kuwa tukio lile linafanana na liliotokea hivi karibuni nchini Saudi Arabia katika msimu wa Hijja ambapo ulikuja upepo mkali na kupelekea kufunuka kwa pazia hilo, jambo ambalo linaashiria kuwa utawala wa SaudI Arabia upo ukingoni mwa uhai wake kutoka na dhuluma zinazofanywa na utawala huo dhidi ya ubinadamu.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky