Iran na Marekani zatishiana vita

Iran na Marekani zatishiana vita

Iran imekuwa ikipambana na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani, Israel, na washirika wao kwa miaka nane sasa, huku Iran ikiendelea kushinda vita hivyo, jambo lililoifanya Marekani kuiongozea vikwazo Iran ili ikose nguvu za kiuchumi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Lugha za vitisho zimetawala kati ya viongozi wa mataifa mawili yenye uadui mkubwa.

Iran imeionya Marekani kuwa ithithubutu kupambana na Iran kwani vita vyake vitakuwa ni vita vikubwa kuliko vita vyote ambavyo Marekani imewahi kuvishiriki.

Nayo Marekani imeionya Iran kuwa itaifanyia uharibifu ambao haijawahi kuufanya kwa nchi yeyote.

Wakati hayo yanajiri Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatullah Ali Khamenei, amesema mazungumzo na Rais Donald Trump "hayana maana" yoyote kwa kuwa Marekani haina tabia ya kuheshimu makubaliano wala saini zake inazoweka kwenye mikataba ya kimataifa.

Akizungumza kwenye mkutano na wanadiplomasia wa nchi yake siku ya Jumamosi (21 Julai), kiongozi huyo mwenye usemi wa mwisho nchini Iran, alirejelea msimamo wake kuhusu Marekani ambao alikuwa nao hata kabla ya makubaliano ya nyuklia kuwekwa saini mwaka 2015. 

"Kama nilivyosema zamani, hatuwezi kuyaamini maneno ya Marekani na hata sahihi yao, kwa hivyo mazungumzo na Marekani hayana maana," aliwaambia wanadiplomasia hao.

"Kudhani kwamba matatizo yanaweza kutatuliwa kupitia mazungumzo au mahusiano na Marekani ni kosa kubwa sana," aliongeza.

Baada ya kujiondoa kwenye makubaliano hayo muhimu ya nyuklia mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani, sasa Marekani ikishirikiana na nchi za kiarabu imepania kuipavikwazo zaidi Iran na kuongeza vikwazo kadhaa vya kiuchumi kuanzia mwezi Agosti.

Ulaya inapingana na hatua hiyo ya Marekani na imeapa kuwa itasaka njia za kuendelea na mahusiano yake ya kibiashara na Iran, ambayo kwa mujibu wa makubaliano iliacha kuendeleza mpango wake wa nyuklia ili nayo iondolewe vikwazo.

Ayatollah Aruhusu mazungumzo na Ulaya kuendelea

"Mazungumzo na Ulaya lazima yaendelee, lakini nao pia hatupaswi kuwasubiria muda mrefu kuleta mapendekezo yao," alisema Khamenei.

Baada ya Marekani kujiondoa kwenye makubaliano hayo ya nyuklia, Iran iliweka wazi kwamba inataka kuendelea nayo, lakini endapo tu mataifa matano yaliyobakia yanaweza kuihakikishia kuwa haitatengwa kiuchumi kutokana na vikwazo ambavyo Marekani na washirika wake wameanza kuvirejesha.

Rais Trump amewahi kunukuliwa akisema kuwa yuko tayari kwa makubaliano mapya ambayo siyo tu yatahusisha mitambo ya nyuklia, lakini pia mpango wa makombora wa Iran na uingiliaji wake kwenye masuala ya Mashariki ya Kati na Ghuba ambao unachukuliwa kuwa kitisho kikubwa dhidi ya mshirika mkuu wa Marekani, Israel.

Iran imekuwa ikipambana na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani, Israel, na washirika wao kwa miaka nane sasa, huku Iran ikiendelea kushinda vita hivyo, jambo lililoifanya Marekani kuiongozea vikwazo Iran ili ikose nguvu za kiuchumi.

Khamenei amuunga mkono Rouhani

Rais Hassan Rouhani mwenyewe ameshakataa maombi manane tafauti ya kukutana na Trump, kwa mujibu wa mkuu wa utumishi kwenye ofisi ya Rouhani. 

Katika hatua nyengine, Ayatullah Khamenei ameliunga mkono onyo lililotolewa awali na Rais Rouhani juu ya uuzaji mafuta. 

Mapema mwezi Julai, Rouhani alisema kuwa endapo usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Iran utatishiwa, basi eneo zima la Mashariki ya Kati nalo litakuwa limetishiwa.

Rouhani hakufafanuwa undani wa onyo hilo, lakini umekuwa msimamo wa muda mrefu wa Iran kwamba itaifunga njia muhimu ya Hormuz ambayo hutumiwa na robo nzima ya meli zinazosafirisha mafuta duniani. 

Mwisho wa habari / 291

 

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky