Iran ndio taifa pekee linaloisaidia Palestina na Lebanon ipasavyo

 Iran ndio taifa pekee linaloisaidia Palestina na Lebanon ipasavyo

Mmoja kati ya wanakamati kuu ya kikundi cha Fatah nchini Palestina ameitaja Jimhuri ya kiislamu ya Iran kuwa ndio nchi pekee inayowasaidia ipasavyo wananchi wa Palestina na Lebanon katika kukabiliana na Israel

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na Abbas Zakiy mmoja kati ya wanakamati kuu ya kikundi cha Fatah, ameashiria kuwa Iran ndio nchi pekee inayowasaidia wananchi wa Palestina na Lebanon dhidi ya uvamizi wa serikali hara mu ya Israel, huku akizitaka nchi za Kiarabu kufanya mazungumzo na Iran kwa lengo la kuwa na umoja baina yao.
Aidha aliendelea kusema hayo alipokuwa katika maadhimisho ya mwaka wa 32 wa kuuwawa kishuja kwa Muhammad Swaleh Husainiy ambaye alikuwa msimamizi wa masuala ya nje wa jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya Iran katika zama hizo nchini Palestina, maadhimisho ambayo yamefanyika jana mjini Birut na kusisitiza kuwa: kipindi tulichopo ni kipindi muhimu pia ni tishio ambapo mataifa ya Kiarabu yanaishi ndani yake, ambapo taifa la Marekani hupandikiza chuki za ubaguzi wa madhehebu au maeneo kwaajili ya kutengeza mpasuko katika mataifa ya Kiarabu na kuyasambaratisha mataifa hayo, kama mauaji yanayoendelea nchini Syria, Iraq na Yemen kwa maana huu wote ni mipango ya ukoroni iliokuwa imepangwa toka miaka mingi iliopita.
Aidha aliongeza kusema kuwa: wale ambao huzitaja ghasia zinazotokea katika mataifa ya kiislamu kuwa ni vita baina ya Shia na Sunni, ni watu ambao wamenunuliwa na Marekani, hivyo basi sisi tunaamini kuwa kuishambulia Hizbullah maana yake ni kuishambulia Lebanon, Palestina na mataifa ya Kiarabu na matakatifu ya kiislamu.       
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky