Iran yapinga vikali masharti ya Marekani

Iran yapinga vikali masharti ya Marekani

Jamhuri ya kiislamu ya Iran imesisitiza kupinga masharti kutoka Marekani ya kuacha kabisa mpango wa nyuklia, kuacha kupambana na magaidi nchini Syria na kuacha kusaidia Lebanon, na nchi nyingine za kiarabu, huku serikali ya Syria, ikitupilia mbali wito wa Marekani kuviondoa vikosi vya Iran nchini humo.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Jamhuri ya kiislamu ya Iran imesisitiza kupinga masharti kutoka Marekani ya kuacha kabisa mpango wa nyuklia, kuacha kupambana na magaidi nchini Syria na kuacha kusaidia Lebanon, na nchi nyingine za kiarabu, huku serikali ya Syria, ikitupilia mbali wito wa Marekani kuviondoa vikosi vya Iran nchini humo.

Ufaransa, mmoja ya mataifa yenye nguvu barani Ulaya, iliosikitishwa na hatua ya Marekani kujiondoa katika mkataba wa nyuklia uliyotiwa saini mwaka 2015, imesema hatua ya Marekani ya kuiongezea vikwazo zaidi Iran, itawaimarisha zaidi wanasiasa wenye msimamo mkali nchini Iran ambao wanaipinga vikali marekani.

Jumatatu wiki hii waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo aliitishia Iran kuwa itakabiliwa na vikwazo vikali zaidi katika historia iwapo haitaachana na ushawishi wake wa kikanda, akiishutumu nchi hiyo kuunga mkono makundi ya silaha yanayopigana na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani katika mataifa kama vile Syria Lebanon na Yemen. Napia Iran inaunga mkono wapalestina dhidi ya waIsrael.

Pompeo aliyasema haya wiki mbili baada ya rais Trump kujiondoa katika mpango wa kimataifa wa nyuklia wa Iran, uliopelekea taifa hilo kuondolewa vikwazo kufuatia hatua yake ya kukubali kusitisha uendelezaji wa mpango huo. Mataifa yenye nguvu barani Ulaya yanauona mkataba huo kama nafasi nzuri ya kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema Pompeo amerejelea shutuma za zamani dhidi ya nchi yake ila safari hii shutuma hizo zimetolewa kwa ukali zaidi. 

Naye afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran Meja jenerali Mohammad Bagheri, amesema Iran haitaisujudia Marekani katika shinikizo lake la kudhibiti shughuli zake za kijeshi. Na kuongeza kwamba Iran haitishwi na nchi yeyote, na itaendelea kupambana na magaidi mpaka hatua ya mwisho, pia itaendeleza kutengeneza silaha na makombola kwa ajili ya kujilinda na kusaidia wanyonge.

 Mjini Paris, Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema hatua ya Marekani kujiondoa katika mkataba huo wa nyuklia na kuiwekea Iran vikwazo itazidisha misimamo mikali na kuhatarisha eneo hilo.

Le Drianamesema Ufaransa itaendelea kutekeleza makubaliano ya mkataba huo hata kama inakubaliana na Marekani kwamba shughuli za nyuklia za Iran pamoja na makombora  zinapaswa kudhibitiwa.

Huku hayo yakiarifiwa Syria imetupilia mbali wito wa Marekani wa kuviondoa vikosi vya Iran nchini humo. Katika vita vya Syria vilivyodumu miaka 8, Iran imekuwa ikitoa msaada muhimu kwa  jeshi la serikali ya Bashar al Assad. Ambapo Marekani na washirika wake wamekuwa wakiyasaidia makundi ya kigaidi ili kuiangusha serikali ya Syria lakini hawakufanikiwa kutokana na msaada wa Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas anatarajiwa kufanya mikutano miwili muhimu hii leo pamoja na maafisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Marekani, ambayo inatazamiwa kujikita juu ya madhara ya kujitoa kwa Marekani katika makubaliano hayo ya 2015.

Mwisho wa habari/ 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky