Iran yawekea vikwazo makampuni 15 ya Marekani yanayodhamini magaidi

Iran yawekea vikwazo makampuni 15 ya Marekani yanayodhamini magaidi

Serikali ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran imeyawekea vikwazo makampuni 15 ya Marekani ambayo yanaunga mkono hatua za kigaidi zinazofanywa na Israel pamoja na magaidi wa Daesh na makundi mengine ya kigaidi yanayofanya jinai zake nchini Syria chini ya udhamini wa Marekani na washirika wake.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali  ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran  imeyawekea vikwazo makampuni 15 ya  Marekani ambayo yanaunga mkono hatua za kigaidi zinazofanywa na Israel pamoja na magaidi wa Daesh na makundi mengine ya kigaidi yanayofanya jinai zake nchini Syria chini ya udhamini wa Marekani na washirika wake.

 Vikwazo hivyo vitakuwa sehemu ya ulipaji kisasi dhidi ya wabunge wa Marekani wanaotangaza kushinikizwa kwa Iran. Uamuzi huo unajiri siku mbili tu baada ya Marekani kutangaza vikwazo vipya dhidi ya wale iliyowalaumu kushirikiana na Iran katika mpango wake wa silaha. Kulingana na taarifa ya wizara na nchi za nje iliyotangazwa na shirika la habari la serikali nchini humo IRNA, vikwazo vya Iran vinazilenga kampuni zinazopatia Israel silaha na vifaa vinavyotumika dhidi ya raia madhulumu Wapalestina na Syria, na kuongeza kuwa zimepigwa marufuku, mali zao nchini Iran zitatwaliwa na maafisa wao hawatapewa visa.

Katika hatua nyingine ya kujibu hatua za uchokozi wa Mareknai, kamati ya bunge la Iran kuhusu masuala ya nje imesema itapendekeza sheria mpya itakayolijadili  jeshi la Marekani na shirika lake la kijasusi kuwa ni makundi ya kigaidi. Tangazo hilo linafuata mswada mpya uliowasilishwa na wabunge wa Marekani kutaka kikosi cha Iran kiitwacho Walinzi wa Mapinduzi au Revolutionary Guards, kuorodheshwa kama kundi la kigaidi. Kikosi hicho cha Iran ndicho kinachosaidia mapambano dhidi ya magaidi wa Daesh wanaodhaminiwa na Marekani nchini Sryia na Iraq pia kikosi hicho kiliongoza vita vya Hizbullah na Israel , vita ambavyo Israel kwa mara ya kwanza ililazimika kusalimu amri na kukubali kushindwa vita.

Iran imechukua hatua hizo kali kama jibu kwa chokochoko za Marekani na vibaraka wake dhidi ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky