Iran:Marekani itajuta kujitoa mkataba wa nyuklia

Iran:Marekani itajuta kujitoa mkataba wa nyuklia

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema kwamba endapo Marekani itajiondoa kwenye mkataba wa nyuklia kati ya nchi yake na mataifa yenye nguvu duniani, basi Marekani itajutia uamuzi huo maisha yake yote.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema kwamba endapo Marekani itajiondoa kwenye mkataba wa nyuklia kati ya nchi yake na mataifa yenye nguvu duniani, basi Marekani itajutia uamuzi huo maisha yake yote.

"Ikiwa Marekani itaondoka kwenye makubaliano ya nyuklia, mtaona hivi karibuni watakavyojutia kuliko ilivyowahi kuwatokezea kwenye historia," alisema mwanamageuzi Rouhani kwenye hotuba yake ya jana Jumapili 6 Mei akiwa kaskazini mwa Iran.

"Trump anapaswa kujua kuwa watu wetu wameunganika, utawala wa Kizayuni (Israel) unapaswa kujua kuwa watu wetu wako kitu kimoja," alisema Rouhani.

"Leo, mirengo yote ya kisiasa nchini Iran, ama iwe kulia au kushoto, wahafidhina, wanamageuzi na watu wa mrengo wa kati, wote wameungana," aliongeza.

Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kujiondoa kwenye makubaliano hayo wakati utakapofika muda wa kusainiwa upya tarehe 12 Mei, akiwataka washirika wa Ulaya "kuyarekebisha makosa makubwa yaliyomo" ama sivyo arejeshe upya vikwazo dhidi ya Iran.

Mkataba huo wa nyuklia ulisainiwa mwaka 2015 kati ya Iran na Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Marekani, wakati huo ikiongozwa na Barack Obama.

Chini ya makubaliano hayo, vikwazo vilipunguzwa kwa masharti ya Iran kutokuunda bomu la nyuklia, lakini Iran inasema haioni mafanikio ya ahadi hizo licha ya kutimiza masharti ya mkataba.

Mara kadhaa, Rouhani amekuwa akirejelea msimamo wa nchi yake kupinga kuzuiliwa nchi yake kuunda makombora yasiyo ya kinyuklia, na hilo amelisisitiza pia kwenye hotuba yake ya Jumapili na kuashiria kuwa Iran itaendelea kujiimarisha katika sekta ya makombora na sekta nyingine za ulinzi.

Naye Trump amekuwa akiukosoa mkataba huo, akitaja baadhi ya vifungu ambavyo anasema vinaondoa vikwazo vya nyuklia kuanzia mwaka 2025.

Rais wa Ufaransa aonya dhidi ya vita

Katika jitihada za kuyaokoa makubaliano hayo, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amependekeza hivi karibuni kwamba mkataba huo usahihishwe na kutanuliwa kuyashirikisha masuala kama hayo yanayolalamikiwa na Trumo, na pia kuondoa kikomo ya muda wa Iran kuruhusiwa kuunda makombora mengine na pia kuangalia dhima ya Iran kwenye eneo la Ghuba na Mashariki ya Kati.

Hatua ya Iran kumuunga mkono Rais Bashara al-Assad, kupitia kundi la Hizbullah la Lebanon, na pia kuwaunga mkono waasi wa Kishia nchini Yemen kumeongeza mzozo kati yake na mataifa ya Magharibi ambayo yanaunga mkono upande wa magaidi na waasi nchini Syria pia yanaunga mkono mauaji  yanayofanywa na Saudia arabia na washirka wake nchini Yemen.

Licha ya hayo, hivi leo Rais Macron ameonya kwamba kunaweza kuzuka vita endapo marekani itajiondoa kwenye makubaliano hayo. 

"Tunaweza kuibua mambo mengine mapya. Kunaweza kukawa na vita," Macron ameliambia gazeti la kila wiki la Ujerumani, Der Spiegel, ingawa ameongeza: "Sidhani kama Donald Trump anataka vita."

Wakati hayo yakijiri Brigedia jeneral Shamhan afisa wa jeshi la wanamaji la Iran amesema : Hakuna uwezekano wa nchi yeyote kuthubutu kuishambulia Iran kwa kijeshi, kwani hatua hiyo itawasha moto usiozimika.

Mwisho wa habari / 291

 

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky