Iran,Urusi na Uturuki kujadili hatima ya Syria

Iran,Urusi  na Uturuki kujadili hatima ya Syria

Iran,Urusi na Uturuki zimejiweka pamoja kuunda nguvu ya muungano wa mataifa matatu wenye lengo la kuimarisha hatua kujiingiza Syria, na kuchukua fursa ya kusitasita mataifa ya magharibi kujiingiza kijeshi nchini humo.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Iran,Urusi na Uturuki zimejiweka pamoja kuunda nguvu ya muungano wa mataifa matatu wenye lengo la kuimarisha hatua  kujiingiza  Syria, na kuchukua fursa ya kusitasita mataifa ya magharibi kujiingiza kijeshi nchini humo.

Marais  wa  mataifa  hayo  matatu , Vladimir Putin , Recep  Tayyip Erdogan , na  Hassan Rouhani  wa  Iran ,  ambao  kwa  muda  mrefu walionekana  kuwa  mahasimu  wa  kimkoa  badala  ya  washirika wa  kimkakati, watakutana  leo  mjini  Ankara kwa  mkutano  wao  wa pili  wa  kilele  kuhusu  Syria  katika  hatua  ya  kuonesha  umoja wao.Mkutano  huu , ambao  unafuatia  mkutano  wa  kwanza  wa  kilele baina  ya  viongozi  hao  mjini  Sochi Novemba  mwaka  jana, unakuja  wakati  Uturuki  ikiwania  kupata  sauti  kubwa  baada  ya kuazisha  mashambulizi  dhidi  ya  wanamgambo  wa  Kikurdi  ndani ya  Syria.

Rais  wa  Marekani  Donald  Trump ameashiria  kwamba   nchi  yake itakuwa  inajiondoa "hivi  karibuni" kutoka  Syria , katika  hatua ambayo  itaimarisha  ushawishi  wa  Uturuki , Urusi  na  Iran   nchi ambazo zimekuwa  na  majeshi  yao  ndani  ya  nchi  hiyo.

Sinan Ulgen , mwenyekiti wa  kituo  cha  sera za  mchanganuo wa mawazo  katika  masuala  ya  kiuchumi  na  sera  za  mambo  ya kigeni  cha  mjini  Istanbul, amesema  mataifa  hayo  matatu sasa yamekuwa  wadhibiti  wakuu  ndani  ya  Syria.

Ulgen  aliongea na waandishi wa habari   kwamba  mataifa  hayo matatu  yamekuwa  "mataifa  yenye  nguvu  kimkoa ambayo  yako tayari  kuwekeza  rasilmali za  kijeshi  kushawishi  matokeo ya mzozo  huo."

Mataifa  hayo  matatu  mwaka  jana  yalianzisha  mchakato wa kuleta  amani  sambamba na  mazungumzo  yanayoongozwa  na Umoja  wa  mataifa  mjini  Geneva. Mazungumzo  hayo , ambayo yanafanyika  Astana, yamefanyika  mara  kadhaa  bila  ya  kupata suluhisho.

Uturuki ambapo nyuma yake kuna mataifa ya kiarabu na mataifa ya kimagharibi wanadhamini upande wa magaidi na wapinzani huku  Iran na Urusi zikiisaidia serikali kupambana na makundi hayo.

Mchakato  wa  wa amani wa Astana

"Mchakato wa  mjini  Astana  ni  chombo ambacho  Uturuki , Urusi na Iran , vinakiangalia  kuweza  kudhibiti  vita  na  kupata  maslahi  yao mbali  mbali," amesema  Elizabeth Teoman , mchambuzi  wa  Uturuki katika  taasisi iliyoko  mjini  Washington  katika  mitaala  ya  vita (ISW).

Urusi ina uwezo  mkubwa  wa  nguvu  za  angani  nchini  Syria wakati  Iran inadhibiti nguvu  za jeshi   la  ardhini ,Lakini  Erdogan ameongeza  ushawishi  wa  Uturuki  kwa  kuazisha mwezi  Januari  mashambulizi  kuukamata  ardhi  kutoka  kwa  vikosi vya  wanamgambo  wa  ulinzi  wa  umma  vya  Wakurdi  vya  YPG.

Mashambulizi  hayo  tayari  yamefanikisha  kukamatwa  kwa  eneo la  zamani  wa  YPG la  Afrin  na  Erdogan  ametishia  mara  kadhaa kuendeleza  msukumo  wake  kuelekea  zaidi upande  wa  mashariki.

"Erdogan  ni  mshirika  dhaifu  kwa  misingi  wa  majeshi  ya  ardhini na  udhibiti  wa  anga. Lakini amejenga  uwiano  na  kuthibitisha kwamba  anaweza  kujenga  uwezekano   ndani  ya  nchi  hiyo," amesema  Teoman.

Lakini  wachambuzi  bado  wana  shaka  juu  ya  uwezekano  wa muda  mrefu  wa  utendaji  wa  muungano  huo  kati  ya  mataifa hayo  makubwa  matatu  ambayo  yametumia  historia  yao  kubwa ya  vita  na  kupigana  vikumbo  kuwania  ushawishi  katika  eneo hilo  la  bahari  nyeusi. Kinadharia  bado wanaendelea  kuwa  katika pande  zinazotofautiana  katika  mzozo  huo , ambapo  Urusi  na  Iran zikitoa  usaidizi  wa  kijeshi  kwa  utawala  wa  Syria  wa  rais Bashar al-Assad   lakini  Uturuki  na wenzake wa Magharibi wanaunga mkono wapinzani na magaidi.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky