Israel: Iran ni lazima itoke nchini Syria

Israel: Iran ni lazima itoke nchini Syria

Waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema: Iran inatakiwa iache kurutubisha yureniam kwakuwa haitajii kufanya hivyo kadhalika inatakiwa iondoke nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Benjamin Netanyahu ameyasema hayo alipokuwa akionga mkono maneno ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani na kusema kuwa: siasa ya Marekani katika kukabiliana na Iran, ndio siasa pekee iliosawa.
Aidha amesema kuwa Iran inachanja mbuga katika kujiendeleza katika nyanja mbalimbali katika ukanda wa mashariki ya kati, ambapo inafanya juhudi kubwa kwaajili ya kupata silaha za Nyuklia.
Benjamin Netanyahu amebainisha kuwa siasa anazotumia Rais wa Marekani dhidi ya Iran, ndio siasa inayopaswa kufuatwa na mataifa mengine, huku akibainisha kuwa Iran inapaswa kusitisha kabisa kurutubisha madini ya Yureniam, kwa sababu hakuna haja yeye kufanya hivyo, pia jambo lingine Muhimu kwa Iran inapaswa iondoke nchini Syria.
Alimazia kusema kuwa yeyete anaetaka kudumisha amani na usalama wa ukanda wa mashariki ya kati, ni wajibu kwake kukabiliana na Iran na kiziunga mkono juhudi za serikali ya Marekani jambo ambalo ndio linalofanya utawala wa Israel.
Warizi wa mambo ya nje wa Marekani amesema kuwa, makubaliano ya Nyuklia ya Iran hayatoi dhamana ya usalama wa ulimwengu, huku akisisitiza kuwa vikwazo vitakavyo iweka Marekani dhidi ya Iran ni vikwazo vizito ambavyo havijawahi kutokea katika historia.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky