Israel: Rais wa Syria ndiye mshindi wa vita

Israel: Rais wa Syria ndiye mshindi wa vita

Waziri wa vita wa Israel akithibitisha ushindi wa Rais wa Syria amesema kuwa kuna safu kubwa ya viongozi wa mataifa ya nchi za kimagharibi na mataifa ya kiislamu, mataifa hayo yote kwa ghafla yanaomba kuwa na uhusiano mwema na serikali ya Syria

Shirika la habari AhlulaBayt (a.s)  ABNA: hayo yamesemwa na waziri wa vita wa Israel na kukiri suala hilo kwa kusema kuwa “Bashar al-Assad” Rais wa jamhuri ya kiarabu ya Syria katika vita ya ndani iliopo ameibuka na ushindi na hivi sasa mataifa mbalimbali yanaomba uhusiano mwema na taifa hilo.
Aliyasema hayo alipokuwa anafanya mahujiano na shirika la habari la Israel na kusema kuwa Bashar al-Assad ameibuka mshindi katika vita ya nchi hiyo huku akisisitiza kwa kusema kuwa kuna safu kubwa ya viongozi wa mataifa ya nchi za kimagharibi na mataifa ya kiislamu, yakiomba uhusiano mwema na serikali ya Syria.
Aidha amesema kuwa tunavita nzito katika kukabiliana na Urusi, Iran na pamona na waturuki na wanamgambo wa Hizbullah, vita ambayo si ndogo na siku hadi siku hali yetu inazidi kuwa mbaya, Mwisho alisema kuwa; wananchi wengi hawalifahamu suala hili, jambo ambalo kwa upande wetu ni zuri, pamoja yakuwa ilikufanikisha jambo hili inahitaji hazina kubwa na kujitolea kwa muda wa masaa 24.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky