Israel yaendeleza ukatili ukanda wa Gaza

Israel yaendeleza ukatili ukanda wa Gaza

Wapalestina wanauawa kwasababu wadai waondolewe mzingiro wa Gaza ambao uliwekwa Zaidi ya miaka kumi, pamoja na haki ya kurejea kwenye eneo hilo ambalo walitimuliwa wakati Israel ilipoanzishwa mwaka wa 1948.
Haya yote yanajiri huku umoja wa mataifa ukiwa umefumba macho na kuziba masikio kuhusu dhulma na unyama unaofanywa dhidi ya wananchi hao, na ikitokea wananchi wa Palestina wakitumia nguvu kudai haki za, wanatangazwa kuwa ni magaidi na wanauawa kinyama.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Majeshi ya Israel yameendelea kufanya mashambulizi makali dhidi ya wananchi wasiojiweza wa Palestina na kubabisha vifo na hasara kubwa.

Wakati hayo yakiendelea Kundi la Hamas limetangaza kusitisha mapigano na Israel katika Ukanda wa Gaza, baada ya siku ya machafuko ambayo yalisababisha vifo vya mwanajeshi mmoja wa Israel na Wapalestina wanne.

Msemaji wa Hamas Fawzi Barhoum amesema kwenye Twitter kuwa makubaliano na Israel yamefikiwa kwa msaada wa Misri na Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa jeshi la Israel amesema hangeweza kuyajadili masuala ya kisiasa, lakini akasema Israel kwa sasa haifanyi mashambulizi yoyote Gaza.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel Jonathan Conriczs amesema jeshi la nchi hiyo tangu Ijumaa liliyashambulia maeneo 60, yakiwemo makao makuu matatu ya wapiganaji wa Hamas.

Jeshi la Israel lilisema mapema kuwa mashambulizi yake ya angani yalikuwa ya kujibu shambulizi la ufyatuaji risasi dhidi ya wanajeshi wake waliotumwa kusini mwa mpaka wa Gaza, ambako waandamanaji wa Kipalestina walikusanyika kwenye uzio wakidai haki yao baada ya kudhulumiwa mji mkuu wao.

Wapalestina wanne waliuawa na wanajeshi wa Israel kufuatia makabiliano yaliyozuka, imesema Wizara ya Afya ya Gaza. Kwa mujibu wa Hamas, ambayo inadhibiti Ukanda wa Gaza, watatu kati ya waliouawa walikuwa wanachama wa Hamas.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov, ambaye hivi karibuni alishirikiana na Misri kupunguza mvutano katika kanda hiyo, aliziomba pande zinazohusika kujizuia na kuwa watulivu. Hapo jana Ijumaa, kulikuwa na maandamano mapya kwenye mpaka wa Gaza, huku Wapalestina wakichoma moto matairi, wakijaribu kueleza hisia zao.

Wizara ya Afya ya Gaza inasema majeshi ya Israel yamesababisha vifo vya Wapalestina 146 na maelfu kujeruhiwa.

Wapalestina wanauawa kwasababu wadai waondolewe mzingiro wa Gaza ambao uliwekwa Zaidi ya miaka kumi, pamoja na haki ya kurejea kwenye eneo hilo ambalo walitimuliwa wakati Israel ilipoanzishwa mwaka wa 1948.

Haya yote yanajiri huku umoja wa mataifa ukiwa umefumba macho na kuziba masikio kuhusu dhulma na unyama unaofanywa dhidi ya wananchi hao, na ikitokea wananchi wa Palestina wakitumia nguvu kudai haki za, wanatangazwa kuwa ni magaidi na wanauawa kinyama.

Vyombo vya habari vya Israel viliripoti kuwa Misri ilituma onyo la mwisho kwa Hamas kutoka kwa Israel, likisema kuwa kama mashambulizi hayatasimama ifikapo wikiendi hii, itafanya mashambulizi mapya ya kijeshi katika ukanda wa pwani.

Hamas na Israel walipigana vita vilivyodumu siku 50 katika mwaka wa 2014. Kwa jumla, Wapalestina 2,250 waliuawa au wakafariki baadaye kutokana na majeraha wakati Waisrael 74 waliuawa katika mgogoro huo.

Iran ambayo ndio msaada mkubwa kwa wapalestina imeahidi kuwasaidia wapalestina na kuhakikisha kuwa taifa la Israel linafutwa katika ramani ya dunia.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky