Jenerali wa Saudia: Iran ni adui zaidi kuliko Israeil

Jenerali wa Saudia: Iran ni adui zaidi kuliko Israeil

Jenerali mmoja wa Saudi Arabia aliyekuwa amestaafu amesema kuwa: utawala wa Kizayuni mpaka sasa hujawahi kufanya tukio lolote dhidi ya serikali ya Saudi Arabia, ama Iran ni adui mkubwa wa Saudi Arabia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na “Anwar Ishqiy” ambaye ni Jenerali aliokuwa amestaafu wa Saudi Arabia alipokuwa anahojiana na Televishen ya BBC akisisitiza kuwa: katika mtazamo wa Saudi Arabia na nchi za uomoja wa Waarabu ni kwamba Israel tuna mashaka kuwa ni Adui yetu, ama Iran ni adui yetu mkubwa.
Aidha akibainisha sababu ya kusema kwake hivyo amedai kuwa: kwani Iran hutuma makomboara na magaidi, ndipo tunampa kipaumbele adui anaetushambulia ukilinganisha na adui tuliekuwa na mashaka naye kuwa ni adui yetu.
“Anwar Ishqiy” amesema kunako ukuwaji wa fungamano la Saudi Arabia na utawala Haramu wa Kizayuni, kuwa Israel hakuna hata mara hujafanya hujuma yeyote dhidi ya Saudi Arabia, hivyo ni adui tuliokuwa na mashaka naye kunako uadui wake.
Alipokukuwa akijibu swali la msimamizi wa kipindi likihusu kwamba utawala wa Israel huwasambaratisha na kuwahujumu wapalestina, alijibu kuwa, Wapalestina si wananchi wa Saudi Arabia, ambapo sisi tunazungumzia adui yetu, hivyo basi muhimu kwetu ni kwamba kujilinda sisi wenyewe kisha kuwalinda ndugu wengine.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky