Jeshi la Israel: vita ijayo dhidi ya Lebanon mlengwa wake ni Hasan Nasrullah

Jeshi la Israel: vita ijayo dhidi ya Lebanon mlengwa wake ni Hasan Nasrullah

Msemaji mkuu wa jeshi la utawala wa Kizayuni amedai kuwa katibu mkuu wa kikundi cha Hizbullah nchini Lebanon ndiye anaelengwa kuuliwa na kusambaratishwa katika vita itakayotokea kati ya Lebanon na majeshi ya utawala wa Kizayuni

Shierika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: msemaji mkuu wa jeshi la Israel ameyasema hayo katika kongamano liliofanyika na vyombo vya habari kuwa: Sayyed Hasan Nasrullah “katibu mkuu wa Hizbullah” nchini Lebanon atakuwa ni mlengwa wa vita itakuwa kati ya Israel na Lebanon ni kumua kiongozi huyo wa Hizbullah.
Aidha ameongeza kusema kuwa majeshi ya Israel yamejitahidi ipasavyo kuonyesha nguvu zake na uwezo wake wa kivita kwa dhahiri na batini ili kuchelewesha vita ijayo, huku akitishia kwakusema kuwa vita itakuwa na tafauti kubwa kwa upande wa pili.
Alimazia kwa kudai kuwa majeshi ya Israel kutokana na ripoti ziliopo yatafanya mashambulizi maalumu dhidi ya Lebanon kwaajili ya kumuua kiongozi wa Hizbullah, ama indapo wakajibu mashambulizi ambayo yataadhiri Israel bila shaka Lebanon itaathirika zaidi.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky