Jeshi la Polisi nchini Nigeria lashambulia waandamanaji na kusababisha vifo na majeruhi 42+ picha

Jeshi la Polisi nchini Nigeria lashambulia waandamanaji na kusababisha vifo na majeruhi 42+ picha

Kwa uchache watu 42 ambao ni wafuasi wa Sheikh Zakizakiy ambaye ni kiongozi mkuu wa kikundi cha harakati ya Kiislamu nchini humo, wamejeruhiwa na kuuwawa katika shambulio liliofanywa na jeshi la Polisi nchini humo katika maandamano hayo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jeshi la Polisi nchini Nigeria lashambulia maandamano ya amani yaliofanywa katika mji wa Kaduna, ambapo kufuatia shambulio hilo watu zaidi ya 40 wamefariki na kujeruhiwa.
Maandamano hayo yalilenga kumtetea Sheikh Zakizakiy, kiongozi mkuu wa kikundi cha Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria, aliokuwa chini ya vyombo vya usalama yeye na mke wake, ambapo majeshi hayo yalishambulia maandamano hayo.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya sehemu hiyo na Nigeria nzima ni kwamba majeshi hayo yalishambulia kwa risasi za Moto na kusababisha vifo vya waandamanaji wawili na wengine zaidi ya arubaini kujeruhiwa.
Baadhi ya watu waliojeruhiwa walikamatwa na majeshi ya Polisi na kupelekwa sehemu isiofahamika, kwa upande mwingine jeshi la Polisi linadai kuwa waandamanaji hao walikuwa wameshika sila za moto na visu, hali yakuwa picha video ziliosambazwa katika mitandao zinaonesha kwamba hawakuwa na silaha yeyote.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky