Jeshi la polisi Nigeria lashambulia waandamanaji/ sheikh apigwa risasi na kujeruhiwa+ picha

Jeshi la polisi Nigeria lashambulia waandamanaji/ sheikh apigwa risasi na kujeruhiwa+ picha

Majeshi ya Polisi nchini Nigeria yashambulia maandamano ya amani ya kumuhami Sheikh Zakzakiy, ambapo jeshi hilo lilitumia mabomu ya machozi katika kuvamia maandamano hayo na kuyasambaratisha

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Polisi nchini Nigeria yameshambulia maandamano ya amani nchini humo yaliokuwa yanafanyika katika mji mkuu wa taifa hilo na kusababisha kujeruhiwa baadhi ya waandamanaji.
Maandamano hayo yalikuwa yalifanyika kwaajili ya kuadhimiasha miaka miwili ya kukamatwa kwa Sheikh Ibrahim Zakizaky ambaye ni kiongozi mkuu wa haraki ya Kiislamu Nigeria pamoja na mke wake, maandamano amabyo yalishambuliwa na majeshi ya polisi nchi humo.
Kufuatia kuvamiwa kwa maandamano hayo watu kadhaa kujeruhiwa ikiwemu Sheikh wa Sokoto Qasim Umari, aidha majeshi hayo yalitumia mabomu ya machozi huku Sheikh wa Sokoto akionekana kupatwa na jaraha kubwa kwa kupigwa risasi ya mguuni.
Habari kutoka kwa mtoto wa Sheikh Zakizaky zinasema kuwa Sheikh Zakizaky yuko katika hali mbaya kiafya naye amepatwa na msituko wa ubongo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky