Jeshi la Saudia laua watoto wa shule zaidi ya 50

Jeshi la Saudia laua watoto wa shule zaidi ya 50

Shambulizi la anga dhidi ya basi la shule lilofanywa na Majeshi ya Saudia arabia jana huko Yemen linaripotiwa kuwauwa watoto zaidi ya 50.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Shambulizi la anga dhidi ya basi la shule lilofanywa na Majeshi ya Saudia arabia jana huko Yemen linaripotiwa kuwauwa watoto zaidi ya 50. Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limeripoti kwamba kufuatia shambulizi hilo la karibu na soko la Dahyan katika mkoa wa kaskazini wa Saada wengi ya waliofariki na kujeruhiwa wamepelekwa katika hospitali inayoisaidia katika utoaji huduma. Shirika hilo limeandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter "Chini ya sheria za kimataifa za kiutu ni sharti raia walindwe wakati wa mapigano." Msemaji wa wizara ya afya iliyo chini ya udhibiti wa Wahouthi Youssef al-Hadri amesema idadi kubwa ya waliouwawa walikuwa chini ya umri wa miaka 15. Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limesema hospitali yake imepokea miili 29 ya watoto huku hospitali nyingine zikipokea miili iliyosalia. Taarifa kutoka kwa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia imesema mashambulizi hayo yalikuwa yamelengwa katika vifaa vya kufyatua silaha zilizotumiwa kushambulia mji wa Jizan kusini mwa Saudi Arabia.

Mwisho wa habari / 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky