Jeshi la Yemen lashambulia mji mkuu wa Saudi Arabia kwa Kombora la Ballistic

Jeshi la Yemen lashambulia mji mkuu wa Saudi Arabia kwa Kombora la Ballistic

Kikosi cha mizinga cha mjeshi ya Yemen yametoa kauli na kutangaza kuwa wamefanya shambulio la kombora la Ballistic katika kambi ya majeshi ya Saudi Arabia iliopo katika mji wa Riyadh

Shirika la habri AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Yemen yamefanya shambulio hilo la kulipiza katika mji mkuu wa Saudi Arabia “Riyadh” ambapo shirika rasmi la habari la Yemen wametangaza wakinukuu kutoka kwa majeshi ya Yemen kuwa jeshi la nchi hiyo kwa mara ya kwanza limefanya shambulio la kombora la Ballistic katika mji mkuu wa Saudi Arabia.
Katika kauli hiyo  iliotangazwa ni kwamba jeshi la Yemen limeshambulia kambi ya majeshi ya Saudi Arabia magharibi mwa mji mkuu wa Saudi Arabia “Riyadh” ambapo lifanyika shambulio hilo kwaajili ya kulipiza mashambulio ya anga yanayofanywa na majeshi ya Saudi Arabia nchini Yemen.
Aidha majeshi ya Yemen yamesema kuwa shambulio hilo pia limefanywa kwaajili ya kutoa ujumbe kwa serikali ya Saudi Arabia kuwa tunauwezo wa kufanya shambulio katika mji mkuu wake bila yakuwa na kikwazo chochote, ambapo kwa mujibu wa ripoti hii, vyombo vya habari vya sehemu hiyo vimesema kuwa kambi iliokuwa imeshambuliwa inaumbali wa kilometa 40 ya mji mkuu wa Riyadh.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Saudi Arabia wameashiria kuwa kombora hilo limefika sehemu ya kambi hiyo bila ya kukosea, huku shirika la habari la Saba la Yemen likinukuu kutoka kwa msemaji mkuu wa kikundi cha Ansarullah nchini Yemen, kuwa kombora hilo limefika sehemu iliokusudiwa ya mji wa Reyadh katika kambi ya kijeshi sehemu ya Al-muzahimiyah.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky