Jumuia ya ushirikiano wa kibinadamu ya Uturuki yakutana na mtoto wa Gaddafi nchini Libya + picha

 Jumuia ya ushirikiano wa kibinadamu ya Uturuki yakutana na mtoto wa Gaddafi nchini Libya + picha

Jopo la jumuia ya misaada ya kibinadamu ya Uturuki waonana na Al-Saadi Gaddafi, ambaye ni mtoto wa Omari Gadafi akiwa na Baghdadi Al-mahmud, ambaye alikuwa waziri mkuu katika kipindi cha mwisho wa utawala wa Gaddafi nchini Libya

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: msafara wa jumuia ya misaada ya kibinadamu nchini Uturuki umeonana na Al-Saadi Gadaafi  na baadhi ya wafungwa wa mambo ya kisiasa nchini Libya katika mji wa Tripoli nchini Libya.
Jumuia ya misaada ya kibinadamu nchini Uturuki imeeliza katika ripoti yake kuwa: jopo la jumuia hiyo limechukua ruhusa kutoka mahakama kuu ya serikali ya Libya ya kuonana na Saadi Gaddafi, mtoto wa Gaddafi, na waziri mkuu wa mwisho wa utawala wa Gaddafi pamoja na Abdallah Sisi ambaye  alikuwa waziri wa ulinzi na usalama katika serikali ya Gaddafi, ambapo walionana nao na kuwajulia hali, ikiwa ni kama moja ya harakati ya jumuia hiyo kibinadamu.
Katika ripoti ya jopo hilo imeelezwa kuwa wafungwa hao watatu wamesema kuwa: hawafanyiwi mambo yaliokuwa kinyume na haki za binadamu ikiwemo kupigwa na kuteswa katika jela hizo, isipokuwa wameikosoa mahakama kuu ya nchi hiyo kwa kuchelewa kutolewa kwa huku yayo nchini humo.
Aidha katika ripoti hiyo jumuia hiyo imeeleza kuwa lengo la kufanya ziara hiyo si kutoa shinikizo kwa serikali ya Libya kwa wafungwa hao, bali ni kujua hali ya kibinadamu ya wafungwa na kuzipatia uvumbuzi chini ya sheria za kimataifa za haki binadamu na kutatua matatizo yanayowezekana kwa wafungwa hao.
Al-Saadi Gaddafi aliondoka nchini Libya kwenda nchini Niger, kabla ya kupinduliwa kwa baba yake nchini Libya mwaka 2011, ama serikali ya Niger baada ya kupinduliwa Gaddafi ilitoa ujumbe kwa haitamrejesha mtoto huyo kwa serikali ya Libya kwa kufuata sheria ya kimataifa ya ukimbizi, lakini baada ya serikali ya Libya kumtuhumu As-Saadi kwa kuwapiga risasi waandamanaji na kushiriki katika makosa mengine katika kipindi cha Utawala baba yake, tangazo la kukamatwa kwake popote atakapokuwepo, kitu ambacho kilipelekea serikali ya Niger kumrejesha Al-Saadi nchini Libya mnamo mwaka 2014.
Alkadhalika Saeful Islamu ambaye ni kaka wa Al-Saadi akiwa na Baghdadi Al-mahmudi aliyekuwa waziri mkuu wa utawala wa mwizho wa Gaddafi na Abdullah Sisi aliyekuwa waziri wa ulinzi na usalama, walihukumiwa kunyongwa na mahakama ya Libya mnamo mwezi Januari mwaka 2015 katika mahakama iliopo mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky