Kamanda Qasim Suleimani awasili nchini Urusi kwaajili ya kuonana na viongozi wa nchi hiyo

Kamanda Qasim Suleimani awasili nchini Urusi kwaajili ya kuonana na viongozi wa nchi hiyo

Kwa mujibu wa ripoti ya Fox News ikinukuu kutoka kwa vyombo vya kijasusi vya Marekani imesema kuwa Qasim Suleimani amewasili mjini Moscow kwaajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wajuu wa nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hilo limetangazwa na Televishen ya Fox News na kudai kuwa kamanda Qasim Suleimani ambaye ndiye msimamizi mkuu wa jeshi la Quds la jamhuri ya kiislamu ya Iran amewasili nchini humo, huku wakisisitiza kuwa kamanda huyo amewasili mjini Moscow pamoja ya kuwepo vikwazo vya umoja wa mataifa dhidi ya Iran.
Aidha Televishen hiyo ikithibitisha madai hayo kwa kutumia mashiko ya vyanzo vya kijasusi vya serikali ya Marekani imeashiria kuwa: Suleimani amewasili nchini humo kwaajili ya kuonana na viongozi wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa madai ya televishen ya Fox News ni kwamba hii ni mara ya tatu kwa kamanda Qasim Suleimani kwenda nchini Urusi kwa mafanya mazungumzo na makamanda wa nchi hiyo.
Msemaji mkuu wa ofisi ya Rais nchini Urusi amesema kuwa hawana taarifa ya safari ya jenerali huyo wa Iran nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky