Kamanda wa Israel: hakuna ishara inayoonyesha kukaribia kusambaratika kwa serikali ya Iran

Kamanda wa Israel: hakuna ishara inayoonyesha kukaribia kusambaratika kwa serikali ya Iran

Kamanda mmoja wa jeshi la utawala haramu wa Israel amesema: serikali ya Iran bado iko mathubuti zaidi na hakuna ishara yeyote inayoashiria kusambaratika kwa Serikali hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na Jenerali mmoja wa jeshi la Israel na kusisitiza kuwa, hali ya serikali ya Iran si kama wanavyosema baadhi ya wanansiasa wanaosema kuwa serikali ya Iran inakwenda ukingoni, bali serikali hiyo kwa sasa bado imara zaidi na haionyeshi alama yeyete ya kusambaratika kwa serikali hiyo.
Aidha aliyasema hayo katika kongamano liliofanyika nchini humo, nakusema kuna baadhi ya wahariri na wanasiasa hudai kuwa serikali ya Iran imedhoofika kufuatia vikwazo walivyo wekewa na serikali ya Marekani, kwa mimi napenda nisema kwamba, serikali ya jamhuri ya Iran hivi sasa iko madhubuti kabisa kuliko kipindi chochote kilichopita, huku akisistiza kushadidi kwa wairan kuuchukia utawala wa Israel.
Kwa upande mwengine amesema kuwa majeshi ya Hizbullah kwa sasa yamekuwa na vifaa kivita imara zaidi kuliko hapo awali na wako tayari kwaajili ya mapambano.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky