Kamanda wa jeshi la Marekani: Albaghdadi inadhaniwa bado yuko hai

Kamanda wa jeshi la Marekani: Albaghdadi inadhaniwa bado yuko hai

Kamanda mkuu wa majeshi ya umoja wa kupambana na magaidi nchini Iraq na Syria amesema: ripoti za kiusalama zilizomfikia kutoka kwa baadhi ya vyanzo vinaashiria kuwepo hai kwa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh Abubakri Al-baghdadiy

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kamanda mkuu wa majeshi ya Marekani maesisitiza kuwa, kutoka na ripoti zinazopingana kutoka kwa majeshi ya Urusi kwamba majeshi hayo kuwa yalifanya shambulio mwezi uliopita ambapo limesababisha kufa kwa kiongozi wa kikundi cha Daesh Abubakari, ama yeye anahisi kuwa badu yuko hai.
Kamanda huyo wa majeshi ya umoja wa kupambana na ugaid nchini Iraq na Syria amesema kuhusu Albaghdadiy kuwa: nahisi kuwa kuongozi huyo bado yuko hai, huku akisisitiza kuwa hakuna vielelzo vyovyote vinavyo thibitisha kifo cha gaidi huyo, kwa upande mwingine kuna vielelezo kadha kutoka idara za usalama zinazoashiria kuwa bado yuko.
Majeshi ya Ururi mnamo mwezi Juni mwaka huu yalitangaza kufanikiwa kumuangamiza kiongozi mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mashambulio kadhaa ya anga waliofanya majeshi hayo pembezoni mwa mji wa Raqqah nchini Syria.
Kamanda wa majeshi ya Marekani amesema alipokuwa anahojiwa na waandishi wa habari katika makao makuu ya majeshi hayo mjini Baghdadi kuwa: umoja wa majeshi ya kupambana na magaidi, kwa muda mrefu umekuwa ukimsaka kiongozi huyo na endapo tukampata, bila shaka tutamuangamiza, huku akisisitiza kuwa: kuna asilimia kubwa inayoashiria kuwa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh yuko katika maficho yaliopo katika mto Euphrates (Furati) nchini Iraq.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky