Katibu mkuu wa NATO aomba bajeti ya ulinzi iongezwe

Katibu mkuu wa NATO aomba bajeti ya ulinzi iongezwe

Katibu mkuu wa shirika la umoja wa kujihami la NATO Jens Stoltenberg anayataka mataifa wanachama kuongeza matumizi yao ya ulinzi

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Katibu mkuu wa shirika la umoja wa kujihami la NATO Jens Stoltenberg anayataka mataifa wanachama kuongeza matumizi yao ya ulinzi katika mkesha wa mkutano wa kwanza kati ya waziri mpya wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis na mawaziri wenzake wa mataifa 27 wanachama mjini Brussels.Stoltenberg alisema leo kwamba ugawanaji uliosawa wa mzigo ongezeko la matumizi katika bajeti za ulinzi ni vitu vitakavyoimarisha umoja huo katika ya mataifa hayo yanayopakana na bahari ya Atlantic. Rais wa Marekani Donald Trump alidokeza wakati wa kampeni ya uchaguzi kwamba huenda asiweze kuyalinda mataifa washirika ambayo yatakataa kuchangia kiasi kinachohitajika kutoka kwao. Matamshi yake yameyashitua mataifa ya Ulaya , hususan yake yaliyoko karibu na mpaka na Urusi kama mataifa ya eneo la Baltic na Poland. wakati huo huo washirika wa NATO wa mataifa ya Ulaya na Canada wameongeza matumizi yao ya ulinzi kwa asilimia 3.8 mwaka jana , ama dola bilioni 10 zaidi kuliko mwaka 2015.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky